Mkuu, kununua gari 0km inabidi kwanza uwe na mind za kifisadi, yaani usiwe na mawazo ya kuionea huruma hela. Pale posta DSM kuna agent wa Toyota anauza Toyota Rumion new model TZS 60m. Sasa mzee kutoa milioni 60 kununua Rumion inahitaji kujizima data, maana ukiagiza Japan iliyotumika kidogo unaipata kwa TZS milioni 30 hivi..yaani hapo kwa agent, Harrier used wanauza milioni 80 na wala sio za umeme, ukiwa na akili za kawaida huwezi nunua. Ni mpaka uwe umeizoea sana hela na una mind flani ya kifisadi, kutoionea huruma hela.