Kununua au kurithi gari mbovu ni jambo ambalo sitamani mtu alipitie.
Una gari lakini wakati wote hauna uhakika wa safari yako.
Upo harusini Mbezi Beach na wewe ni mkazi wa Pugu Kajiungeni, unakunywa na kula huku ukifurahi lakini ukikumbuka kuwa gari yako spana mkononi furaha yote inapotea.
Maana harusi ikiisha unaweza kwenda kwenye gari na isiwake, inaweza ikawaka lakini ikaja kuzima Mwenge na ni usiku.
Kama sio fundi na hutaki kuchanganyikiwa na kujiingiza kwenye gharama zisizo na mwisho, tafadhali usinunue gari mbovu wala usikubali kurithishwa gari mbovu.