Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku yako ni njema.!
Unae Mungu muweza wa yote.

Yeremia 32:27
[27]Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiliweza?

Hakuna lililogumu kwako, hakuna jaribu lililo juu ya nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yako.
Mungu anakuthamini sana hata amekupa siku ya leo akiwa na uhakika wa kukutunza na kukuwezesha katika yote unayoyapitia. Kaa ndani yake nae atakufanikisha kwakua mapenzi yake ni mema.

MUNGU ANAKUWEZESHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa! Ni asubuhi njema tumeiona kwa neema na baraka za Mungu. Hivyo nikutie moyo kwa ujumbe toka Warumi 12:15-16

*"Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili."*

Mtume Paulo anatukumbusha ktk maisha yetu ya ufuasi kwa Kristo ni sharti tujihusishe na watu wote ktk furaha na mateso yao.

Kujihusisha kwa jinsi hii ni alama ya upendo wa kweli, na huko ndiko kutenda haki na huruma.

*Aidha kila mtu ana wajibu wa kuishi maisha ya kupatana, tusiwe watu wa majivuno bali tuishi kwa unyenyekevu na kushirikiana na watu wote.*

MUNGU AKUBARIKI!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amina!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…