Biryani ya kuku rahisi Mahitaji Mchele Mchele 1/2kilo Karafuu vipande 6 Mdalasini vipande 4 Iliki nzima 4 Chumvi kiasi Maji Kuku Kuku mzima 1 Vitunguu maji 4 Vitunguu saumu 1 tsp Tangawizi 1 tsp Giligilani ya unga 1/2tsp Binzari manjano 2 tsp Pilipili manga 1/2 Maziwa mgando kikombe 1 Limao 1 Nyanya 4 Garam masala 1tsp Mafuta na chumvi Njia Mchele wako loeka km lisaa moja na kisha chukuwa uweke kwy maji na chumvi,iliki,mdalasini na karafuu uchemshe kisha uchuje na weka pembeni Kwy sufuria jingine chukuwa mafuta weka vitunguu vyako acha vipate rangi ya kahawia kisha weka kuku, vitunguu saumu,tangawizi,giligilani ya unga, pilipilimanga,binzari na garam masala na chumvi acha ichemke weka nyanya zako na funika ziive vizuri na mchanganyiko uive kisha weka maziwa yako ya mgando koroga na acha ichemke vizuri na iwe na uzito kisha weka limao Kwy sufuria jingine anza kwa kuweka huu mchanganyiko wa kuku kisha weka wali rudia tena kwa kuweka mchanganyiko wa kuku na malizia wali kwa juu kisha nyunyizia mafuta kidogo palia na mkaa juu na chini au weka kwy moto mdogo kwy gesi uufunike na mfuniko unaobana vizuri. Acha kama dakika 20 epua na uchanganye vizuri na upakuwe tayari kwa kuliwa.