Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuku wa kuchoma Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu 1 tsp Tangawizi 1 tsp Limao Binzari ya manjano 1/2 tsp Garam masala 1/2 tsp Curry powder 1/2 tsp Chumvi Mafuta vijiko 2 Njia Chukuwa kuku muweke mahitaji yote kitunguu saumu, tangawizi,limao,binzari ya manjano,garam masala,curry powder,chumvi na mafuta na mpake hakikisha anaingia vizuri kwy kuku na kisha muweke kwy friji chini kwa muda wa saa 6 au hata usiku mzima Kisha washa oven 200°c na muweke kuku wako kwa muda wa saa 1 kisha mpasue katika ili kumfungua ili achomeeke vizuri kwa ndani kwa muda wa dk 35 na tayari na hakikisha anapata yangi nzuri ya kahawia. Enjoy unaweza kula na chochote ni mtamu sana
 
Nyama ya mbuzi choma (simple) Mahitaji Nyama ya mbuzi kilo moja Kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai Tangawizi kijiko kimoja cha chai Limao moja Chumvi Mafuta vijiko viwili Njia Chukua nyama yako weka viungo vyote kitunguu saumu, tangawizi limao,chumvi na mafuta na unahakikisha viungo vyako vinaingia vizuri kwy nyama Kisha weka funika na weka kwy friji kwa masaa 7 au usiku mzima ili viungo vyako viingii vizuri kwy nyama Kisha bake 160°c kwa masaa 2 au unaweza kuchoma kwy jiko la mkaa lenye wavu juu kwa masaa mawili hakikisha moto ni mdogo ili aive vizuri. Tayari kwa kula
 
DAGAA WA NAZI NA MAZIWA Mahitaji Dagaa wa mwanza robo kilo Kitunguu maji 1 Nyanya 3 Pilipili hoho nusu Karoti 1 Tui la nazi zito 1/2kikombe Maziwa fresh 1/2 kikombe Kitunguu saumu na tangawizi1/4kijiko cha chai Royco 1 kijiko Beef masala 1 kijiko Binzari ya manjano1/4kijiko Mafuta kiasi Chumvi kiasi Njia Chukuwa sufuria weka mafuta subiri yachemke kisha weka kitunguu kaanga kidogo kisha weka vitunguu saumu na tangawizi endelea kukaanga upate rangi ya kahawia kisha weka karoti pilipili hoho na nyanya endelea kukaanga kisha weka dagaa zako na weka maji au tui la pili km umetumia nazi ya kawaida kisha weka dagaa zako Baada ya hapo weka viungo wako royco binzari na beef masala na chumvi na ongeza maji au tui la pili funika acha ive kwa muda ukishaona imeiva weka tui lako na maziwa acha kwa muda kidogo. Epua na tayari kwa kuliwa haswa na ugali Enjoy
 
PILAU YA NYAMA YA KUSAGA MAHITAJI mchele vikombe 2 Nyama ya ngombe ya kusaga 1/4 kilo Njegere kiasi Kitunguu maji 3 Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai Tangawizi nusu kijiko Pilau masala kijiko kimoja Curry powder 1/2 kijiko Royco 1/2kijiko Beef masala1/2 kijiko Mafuta ya kupikia na chumvi Kachumbari Kitunguu maji 1 Nyanya 2 Tango nusu Limao 1/2 Pilipili 1 Njia Weka mafuta kiasi jikoni kisha weka vitunguu subiri vianze kubadili rangi kisha weka kitunguu saumu na tangawizi baada ya hapo weka njegere ulizozichemsha pembeni na nyama acha kwa muda kidogo kisha weka viungo wako pilau masala,curry powder,royco,beef masala na chumvi kisha acha viungo viingii vizuri kwy nyama ya kusaga na viive kisha weka mchele wako na ongeza maji ya moto kiasi kulingana na mchele wako funika na acha mpk pilau likaukii kw moto wa wastani Kachumbari Katakata vitunguu osha na chumvi na maji kiasi kuondoa ukali kisha katia nyanya na tango kwa style yote upendayo kisha weka chumvi,pilipili na limao changanya tayari kwa kuweka kwenye pilau letu Kwa wapenzi wa mayonase unaweza ukaongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…