Unaweza tumia scrub ili kurainisha ngozi yako na kuifanya iwe inavutia. Scrub zipo za aina nying ila zilizotengenezwa kwa mimea asili au matunda ndio nzuri zaidi. Unaweza tumia scrub ya mawese au unaweza tengeneza kwa kutumia machicha ya nazi ambayo hurainisha ngozi yako na kuiacha ikiwa inavutia na kung’aa kwa uhalisia. Pia unaweza tumia scrub ya mchanganyiko wa asali na maziwa ambapo unachukua vijiko viwili vya chai vya asali unachanganya na maziwa kidogo tuu alafu unachemsha pamoja , vikipoa paka usoni na kaa kwa dakika kama tano ndipo uoshe uso wako.