Tabasamu la kila mmoja kati yetu hutegemea usafi wa kinywa chake unaotokana na kupiga mswaki na kusugua kwa umakini. Changamoto iliyopo ni namna ya kufanya hivyo kwa ufasaha.
Wengi hawafahamu njia sahihi za kupiga mswaki kwa ajili ya afya ya kudumu ya kinywa inayoaanza hapo. Kinywa safi ni msingi wa afya njema ya mwili.
Afya ya kinywa inaanza na meno yaliyo safi. Hili hufanyika kwa kutunza maeneo na meno yanakutana na fizi katika hali ya usafi huzuia magonjwa ya fizi na kuzuia kutoboka kwa meno.
Kulingana na umri, mazingira au hali ya afya, unashauriwa kutumia mswaki sahihi utakaokufaa pamoja na dawa ya meno iliyo na madini ya floridi. Mswaki mzuri ni ule ambao visafishio vyake havikuumizi na unaokaa vizuri kinywani.
Kanuni ya tatu ni kujizoeza njia nzuri za kupiga mswaki. Unapaswa kuushika mswaki wako kwa namna ambayo visafishio (brashi) vyake vitalenga kwenye makutano ya meno na ufizi.
Unachotakiwa kufanya ni kusafisha meno yako kwa mwendo mfupi wa kwenda mbele na nyuma, juu na chini. Kumbuka kusafisha nje, ndani na sehemu za kutafunia. Halikadhalika usisahau kusafisha ulimi kwa kutumia mswaki wakati ukipiga mswaki.
Kama una miswaki kadhaa na yote unaitunza mahali pamoja, tenganisha huu uliotumia sasa na hiyo mingine ili kuzuia maambukizi ya bakteria. Weka mswaki wako mahali penye hewa ya kutosha vinginevyo huweza kuchochea ukuaji wa bakteria na fangasi kwenye mswaki wako ambao wanaweza kukusababishia maambukizi ya mgonjwa ya kinywa au mwili kwa ujumla
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.