Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Niliwahi kumfahamu jamaa fulani aliyekuwa akifanya kazi wakata wote, isipokuwa alipolala. Alikuwa akiamka alfajiri na kukamua maziwa ya ng’ombe wake na kusafisha zizi. Kisha aliondoka kuelekea kazini akipitia kwenye mradi wake wa duka na kuhakikisha linafunguliwa.
 
Wakati wa mapumziko kazini alikuwa anachukua maziwa aliyokamua asubuhi na kuyapeleka kwa wateja wake. Baada ya saa za kazi alielekea nyumbani huku akipitia dukani kwake kuangalia mahesabu. Kisha alikwenda haraka nyumbani kukamua maziwa na kuhakikisha mifugo imefungiwa zizini.
 
Kwa jinsi jamaa huyu alivyokuwa akifanya kazi, watu walimwita Bwana Kazinyingi. Hakuwa na muda wa kukaa na kuongea na mkewe na watoto wake. Ingawa alikuwa na nyumba nzuri, fanicha bora na vifaa vya kisasa kama vile televisheni, video na vinginevyo, kamwe hakuwa na muda wa kuvifaidi.
 
Kwa jinsi alivyojifanya alikuwa mtumwa wa kazi, hakuwa na amani wala furaha. Baada ya muda alisumbuliwa na maradhi kadha wa kadha kama shinikizo la damu, msongo wa mawazo, vidonda vya tumbo na mwisho alipata kiarusi akapooza na hakuweza kuendelea na kazi zake alizozizoea.
 
Hili ni moja kati ya matatizo yanayowakabili watu wengi katika maisha. Huwa hawafikiri kuwa kupumzika ni jambo muhimu kwa binadamu. Kuna mtaalamu mmoja alifanya utafiti katika baadhi ya nchi zinazoendelea. Aliwahoji watu wengi ili kujua kama katika maisha yao huwa wanapumzika.
 
Kuna baadhi walisema labda wanaweza kuanza kupumzika wakati watoto wao watakapokua wakubwa na kuanza maisha yao wenyewe. Kuna wengine, hususan wafanyakazi walisema huenda watapumzika watakapostaafu. Bado kuna wale waliosisitiza kuwa kupumzika ni kustarehe, hivyo watapumzika tu watakapokuwa wamepata yale yote wanayoyatarajia katika maisha yao kama vile kujenga nyumba, kuwa na shamba au kununua vitu muhimu katika maisha kama gari, fanicha na vitu vinginevyo muhimu.
 
Pombe pia huwa ni chanzo cha mtu kulala haraka lakini husababisha kushindwa kupata usingizi mzuri na kusababisha mtu kuamka mara kwa mara nyakati za usiku.
Dr nakusalimia...ama baada ya salamu naomba niulize mimi sijanywa kahawa,sina msongo wa mawazo na pombe sijanywa ila sijapata usingizi tatizo ni nini[emoji22][emoji22]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…