Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

98989d15029b15c3b025d10133507d7e.jpg
 
Tulio wengi tunaishi kama kwamba tuna mkataba wa kutekeleza kila jambo linalotukabili. Tunachelewa kulala, tunaamka mapema, tunakosa muda wa kujiburudisha na kustarehe na familia zetu tukiamini siku moja shughuli zitakwisha. Jambo hili halitatokea daima kwa sababu kila tunapokamilisha jambo moja linatokea jingine badala yake.
 
Aidha, tukumbuke kuwa lengo la kuishi siyo kutumia wakati wetu wote katika shughulikia maisha bila kuhakikisha tunaishi kwa furaha, amani na utulivu. Ni dhahiri kuwa tunawajibika kuwa na hali ya kufanikiwa na kufanya kazi kwa juhudi zote, lakini tukifanikiwa kuziliwaza mbongo na kuburudisha miili yetu, tutaweza kuzifanya fikira zetu ziwe makini zaidi na kupata matokeo bora zaidi. Tukijizoeza kupumzika walau kidogo kila siku, tutastaajabu jinsi tutakavyoweza kufanya kazi kwa makini zaidi na kwa kiwango kikubwa bila kuchoka.
 
Kwanza, tuwaonye wale wanaofikiri kuwa katika maisha kuna wakati unaofaa kupumzika, kwa kuwa kupumzika ni sehemu ya maisha. Pia inabidi tukumbuke kuwa muda wa kupumzika hauji wenyewe ila ni sisi tunaowajibika kutafuta wasaa wa kupumzika walau kidogo kila siku. Siyo vyema kuijaza kila siku kwa kazi nyingi kama yule rafiki yangu Bwana kazi nyingi.
 
Mwisho tufahamu kuwa kupumzika ni pamoja na kupata usingizi wa kutosha. Wataalamu husema binadamu anahitaji muda usiopungua saa nane za kulala kila siku. Ili kuwa na utaratibu mzuri wa kuishi kwanza hakikisha una afya nzuri na boresha uwezo wa kufanya kazi wa mwili wako kwa na mapumziko na kufanya mazoezi.
 
KULA CHAKULA KINGI

Kula zaidi nyakati za usiku ni kero kwa hiyo, ulaji wa chakula kidogo kabla ya kulala ni jambo zuri lakini kula chakula kingi nyakati hizo huleta mtu kushindwa kukaa kwa raha wakati wa kupumzika kitandani na hivyo kushindwa kupata usingizi.
Mlo kama huu unaukamata saa nne usiku ndo unakwenda kulala unategemea nini?
d6f9f6c2f5fb9df1c1a152b7eec39d56.jpg
 
Back
Top Bottom