2. Chukua beseni zako za kufulia weka maji masafi, beseni moja ni la kufulia, jingine la ku suuzia. Weka sabuni yako ya unga kwenye beseni la kufulia, kisha ichanganye kwa mkono mpaka itoe povu, halafu dumbukiza nguo zako na kisha anza kufua. wakati wa kufua unazingatia maeneo ya kola, makwapa, kama ni kanga kwenye pindo, kama nguo ina mifuko, basi kwenye mifuko, na pia kwenye pindo za suruali. unapaka sabuni ya kipande kwenye hayo maeneo na kusugua vizuri. kisha unaishika nguo kama unaitandaza na kuisugua randomly kila upande.