Tembea haraka zaidi
Utafiti unaonyesha kuwa hali na hisia za mtu huweza kutambulika kutokana na mkao wake, jinsi anavyosimama na anavyotembea.
Mtu anaposimama kiuchovu au anapotembea kigoigoi, huonekana waziwazi kuwa ana hisia dhaifu kuhusu haiba yake, yeye mwenyewe na watu wengine, pia mtazamo wake kuhusu kazi na maisha ni hasi.