Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vivyo hivyo utajisikia kuwa wewe ni jasiri iwapo utasimama kwa ukakamavu kuliko ukisimama umelegealegea. Kwa hakika vitendo hutawala hisia zetu. Kwa mfano mtu anayeona aibu kujitambulisha kwa mtu ambaye amekutana naye kwa mara ya kwanza na ambaye ni lazima ajitambulishe kwake, anaweza kubadili aibu ama woga wake ukawa ujasiri kwa vitendo. Anaweza kufanya vitendo vitatu sambamba. Kwanza atoe mkono kwa mtu huyo anayetaka kujitambulisha kwake na kukishika kiganja cha mtu huyo kwa ukakamavu. Jambo hili linapotokea liende sanjari na kumtazama mtu huyo usoni na kusema maneno ya kujenga mazingira ya mawasiliano kama vile “nimefurahi kukutana na wewe”. Vitendo hivi vitatu vitasaidia kuondoa kabisa woga na kuweza kujitambulisha.
 
Kama ambavyo tumeona, vitendo huweza kujenga hali ya kujiaminina kutenda kile unachohisi huwezi. Hivyo, ili uweze kufikiri kwa kujiamini, fanya vitendo vinavyoendana na jinsi unajihisi. Lakini kuamua na kutenda vitendo vinavyojenga hali ya kujiamini siyo jambo rahisi. Tabia hii itaweza kujengeka kwa mazoezi ya muda mrefu na dhamiri ya dhati na zaidi ya yote kuthubutu. Kuna njia na mbinu nyingi ambazo watu wamezitumia na zikawafaa kama ifuatavyohaya yafuatayo:-
 
Thanks for the [emoji116][emoji116]


1e3bea37b252dceb7b5c3c9bbc097976.gif
 
Kaa katika safu ya mbele

Mara nyingi tunapokwenda kwenye kumbi za shughuli au mikutano huwa tunaona viti vya nyuma ndivyo ambavyo huanza kujaa kwa kukaliwa na watu.

Wengi hupendelea kukaa kwenye viti vya nyuma ili wasionekane moja kwa moja. Kinachofanya waogope kuonekana ni hulka ya woga na kutokujiamini. Kumbuka kukaa kwenye safu ya mbele ukumbini husaidia kujenga uwezo wa kujiamini. Tangu sasa ifanye iwe tabia yako kukaa kwenye safu ya mbele au karibu na safu hiyo.
 
Jizoeze kukutanisha macho na unayewasiliana naye

Jinsi mtu anavyoyatumia macho yake wakati anapokuwa mbele ya watu huweza kuonyesha jinsi alivyo. Unapozungumza na mtu ambaye hakutazami machoni huwa hujiulizi maswali kama vile. “Anajaribu kuficha nini? Anaogopa kitu gani? Je kuna jambo ambalo hataki litambulike kutokana na jinsi anavyoonekana?
 
Mtu anaposhindwa kukutanisha macho yake na anayeongea naye huashiria mambo mawili; kwanza, hujionyesha kuwa yeye ni wa hali ya chini kwa yule anayeongea naye.

Pili, huenda anaficha kosa fulani alilofanya, hivyo anaohofu yule anayeongea naye ataweza kulibaini. Kwa kutazama macho ya mtu, askari au hakimu huweza kutambua kama mtu ametenda kosa au anasema uongo au kweli
 
Back
Top Bottom