Leo kwa ufupi tumfahamu nyoka aitwae “KIFUTU” Kuna aina nyingi sana za nyoka hawa jamii ya kifutu duniani na hasa hapa kwetu Tanzania pia. Sasa nadhani itakuwa vizuri tukichagua jamii moja ya kifutu nakumueleze ambae ni “KIFUTU MSITU”
KIFUTU MSITU ndio kifutu mkubwa kuliko jamii nyingine za kifutu wapatikanao barani Afrika. Sio tu nio mkubwa kwa jamii za vifutu wapatikanao barani Afrika bali pia ndio anaongoza kwa uzito kuliko vifutu wote duniani. Nyoka huyu barani Afrika anapatikana nchi mbalimbali kama Guinea, Ghana, Togo, Nigeria, Cameroon, Equatorial Guinea, Gabon, DR Congo, northern Angola, Jamuhuri ya Arika ya Kati, South Sudan, Uganda, Kenya, kusini mashariki mwa Tanzania, Zambia, Malawi, mashariki mwa Zimbabwe, na Msumbiji .