ANGALIZO: Ukimaliza kusoma hii habari, kimbilia kiporo chako cha wali na maharage na ukile hadi ukinai, maana ni habari njema kwa wale wanaopenda kula bila kuongeza kilo kwenye miili yao.
Kuwa makini tu jinsi ya kupasha moto.
Kula vyakula vilivyotoka kuandaliwa ni salama na afya zaidi, hii haina ulazima wa ufafanuzi.
Lakini kuna jamii ya vyakula ambavyo ni vizuri zaidi kula vikiwa kama viporo.
Aina mojawapo muhimu sana la hivi vyakula ni kundi la vyakula vya wanga (carbohydrates).
Tunakula vyakula vya wanga mara nyingi sana kwenye milo yetu ya kila siku.
Ukila vyakula vya jamii ya wanga unaongeza kiwango cha sukari kwa kasi sana kwenye damu, wakati wa mmeng'enyo, hivyo hulazimu mwili kufanya kazi ya ziada ya kutoa kimeng'enyo cha insulin kinachofanya kazi ya kupunguza sukari kwenye damu.
Hii kupanda na kushuka kwa damu kwa kasi husababisha chakula kusagwa haraka sana na unaweza kusikia njaa muda mfupi baada ya kula.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.