Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.
Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.
Zabibu pia zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo na hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mkojo unaotengenezwa na figo.
Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili.
Hali kadhalika zabibu pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.