Wangapi ughaibuni wanafuatilia Es Setif ya Algeria, washindi wa klabu bingwa za Afrika sasa hivi ? Ni idadi gani ya wapenzi wa soka wanaochangamkia mashati na kutundika bendera za timu hiyo muafaka inayobeba rangi mbili za mistari meusi na meupe?
Lakini tulisikia Mkenya, Suleiman Alphonso Omondi, alivyojinyonga miaka sita iliyopita baada ya Arsenal kutolewa nje ya michuano ya klabu bingwa za Ulaya (Champions League), kwa kudundwa mabao 4-1 na wapinzani wao wa kijadi, Manchester United.