Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tukae sasa mezani tukionja sambusa na mandazi ya mwaka wetu huu mpya wa 2015.

Mwaka ulioanza na kunguru na siafu. Habari za tafrani za Panya Road kutisha baadhi ya wananchi jijini Dar es es Salaam na kupigwa risasi mtuhumiwa wa muuza dawa za kulevya, kutoka Sierra Leone, Abdul Koroma.
 
Picha za vurumai hizi zimeshtua. Wakati huo huo, wiki jana wakati wa michuano ya ligi ya Uingereza baina ya Arsenal na Southampton, (timu ndogo sana iliyokuja juu 2013) Arsenal ilichomwa jambia la 2-0. Picha ya mshabiki wa Kitanzania aliyezimia kavalia jezi la Arsenal ilisambazwa mitandaoni. Wengine walidai mlevi, wapo wanaokiri walimwona. Akisononeka.
 
Wangapi ughaibuni wanafuatilia Es Setif ya Algeria, washindi wa klabu bingwa za Afrika sasa hivi ? Ni idadi gani ya wapenzi wa soka wanaochangamkia mashati na kutundika bendera za timu hiyo muafaka inayobeba rangi mbili za mistari meusi na meupe?

Lakini tulisikia Mkenya, Suleiman Alphonso Omondi, alivyojinyonga miaka sita iliyopita baada ya Arsenal kutolewa nje ya michuano ya klabu bingwa za Ulaya (Champions League), kwa kudundwa mabao 4-1 na wapinzani wao wa kijadi, Manchester United.
Numbisa ni maandishi ya Nani haya
Sio yule mkenya

CantstopwontStop
 
Picha za vurumai hizi zimeshtua. Wakati huo huo, wiki jana wakati wa michuano ya ligi ya Uingereza baina ya Arsenal na Southampton, (timu ndogo sana iliyokuja juu 2013) Arsenal ilichomwa jambia la 2-0. Picha ya mshabiki wa Kitanzania aliyezimia kavalia jezi la Arsenal ilisambazwa mitandaoni. Wengine walidai mlevi, wapo wanaokiri walimwona. Akisononeka.
 
Klabu iliyovumbuliwa mwaka 1907 ni rika moja na za Ulaya na Marekani ya Kusini. Real Madrid ilizinduliwa 1902, Manchester United, 1902, Chelsea 1905, Bayern Munich 1900, Santos ya Brazil, 1912.

Al Ahly imeshatajwa kuwa klabu kubwa kuzidi zote za Afrika baada ya kushinda kombe la CAF mara nane toka kimbunga hicho kilipozaliwa 1964.
Mbona mifano yake ya ulaya tena

CantstopwontStop
 
Chelsea na Tottenham nazo zikapambana. Chelsea (inayoongoza ligi hii sasa) ikababuliwa 5-3. Baada ya matokeo haya ya kusisimua, kila aina ya utani na picha vilienezwa magazetini, katuni, mablogu, mitandao na simu za viganjani.

Ipo iliyomsanifu kocha Jose Mourinho akichungulia, akijiuliza wapi ajifiche; wapo walioizomea au kuililia Chelsea. Taswira iliyopiku ni ile ya mshabiki wa Chelsea akilia kama mtoto mdogo huku kakumbatiwa na kuliwazwa na mwanamume mwenzie.
 
Kwa nini Waafrika tuko tayari kulia, kuzimia, kujiua kwa timu zilizo mbali sana wakati wenzetu hawatufahamu wala kutujali? Nini hasa msingi wa tatizo? Labda maliwazo, mlizamu, mnato, njaa, kiu na raghba tuliyo nayo kwa vitu vya ugenini hutokana na sisi wenyewe kutomudu mambo yetu? Je, tunakiri kuwa, “Siri ya kuheshimiwa” ni pale unapojipenda (sana), mwenyewe? Ukishajipenda, kujivuna na kujiheshimu, hata wasiokujua wataliimba jina lako na kuweka picha za wapenzi na masahiba zako ukutani.
 
Back
Top Bottom