Kubaliana na ukweli kwamba kuna mambo huwezi kuyabadili. Ubinadamu una mipaka. Kuna ambayo tunaweza kuyafanya au kuyabadilisha. Litizame jambo linalokupa msongo wa mawazo kwa makini. Je,lipo ndani ya uwezo wako? Kama halipo, usihangaike. Muachie Mungu. Badala yake pambana kubadili yale ambayo yapo ndani ya uwezo wako. Kuna msemo wa kiingereza huwa naupenda; Sometimes the best thing you can do is not think, not wonder,not imagine,not obsess.Just breathe, and have faith that everything will work out for the best.