Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kubali Mabadiliko– Dunia ya leo inabadilika kila siku na kwa kasi sana. Kuna mambo ambayo yanaweza kukukwaza. Yapo mambo ambayo yanaenda kinyume kabisa na imani zako. Kubaliana na hali halisi. Sio lazima ushiriki moja kwa moja katika mabadiliko. Kubaliana tu na ukweli kwamba mambo yanabadilika. It is what it it is.It was what it was.It will be what it will be.Don’t stress it.
 
4177.jpg
 
Panga Ratiba Zako Vizuri– Miongoni mwa mambo ambayo husababisha stress ni pamoja na kutopangilia muda au ratiba vizuri. Kwa mfano unapojishtukia asubuhi umechelewa kuamka, ni wazi kwamba moyo wa wasiwasi huanza kukuenda mbio. Una-panic. Matokeo yake ni kwamba mambo mengine mengi yatakwenda kombo. Chukua dakika 10 au 15 usiku kuandaa kesho.
 
Kwa mfano, chagua nguo utakazovaa usiku. Weka kila kitu unachotakiwa kutoka nacho kesho kwenye aidha pochi au begi lako. Kama huwezi, na kuna kitu unataka kukumbuka asubuhi, jitumie ujumbe mfupi wa maneno (text) kwenye simu yako. Ukiamka bila shaka utachukua simu yako. Itakukumbusha.
 
Kuwa Makini Katika Kuchagua Marafiki– aina ya marafiki waliokuzunguka wanaweza kuwa chanzo cha furaha au karaha. Wanaweza kuwa chanzo cha msongo wa mawazo. Chagua aina ya marafiki ambao watakusaidia kusonga mbele. Rafiki anayekukatisha tamaa kila siku,sio rafiki. Achana naye. Rafiki asiyekupa issues za maendeleo ni “adui”.Muepuke. The people in your life should be a source of reducing stress not causing more of it.
 
Jicheke wewe mwenyewe-Kumbuka kujicheka wewe mwenyewe hususani pale unapofanya makosa. Badala ya kujipiga kichwa Ukutani au kujipiga kwenzi, jitizame kwenye kioo ujicheke. Jikumbushe kwamba wewe ni binadamu usiye kamili. Unakosea.
 
Usiseme NDIO kwa kila kitu au kila jambo– Baadhi yetu huwa hatupendi kuonekana “wabaya”. Tunajaribu kumridhisha kila mtu. Unasema NDIO kwa kila ombi au jambo. Matokeo yake unatingwa na mambo mengi kwa mpigo ambayo kibinadamu huwezi kuyatimiza yote. Usikubali kila kitu. Wala usijisikie vibaya kusema HAPANA.
 
Back
Top Bottom