Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Naunga mkono hoja [emoji817][emoji817][emoji817][emoji817][emoji817][emoji817]
 
Soma Kitabu– Hii ni mojawapo ya mbinu ambazo mimi binafsi huzitumia sana pindi mambo yanapokuwa magumu. Huchukua kitabu kizuri cha hadithi(novel) na kujizikia humo nikisoma. Waandishi ninaowapenda zaidi ni kama Lee Child, John Grisham, J.D Robb, James Patterson, Tom Clancy na David Baldacci.
 
Pata Usingizi Wa Kutosha– Binadamu wa kawaida anatakiwa kupata muda wa masaa 6 mpaka 8 ya kupumzika(kulala). Kinyume chake, unakuwa unajiandaa kwa hatari za kiafya na pia msongo wa mawazo. Mtu ambaye hajapumzika vizuri ni mwepesi wa kughafilika. Atahamaki hata kwa mambo madogo tu. Hamaki huzusha mikasa na hugombanisha watu. Athari za kutopata usingizi wa kutosha na mbinu za kufanya ili kulala(hususani unaposhindwa kulala kutokana na mawazo nk) nitaziongelea siku moja.
 
Chagua Kuwa Mwenye Furaha– Muumba ametupa uwezo wa mambo mengi sana. Mojawapo ni uwezo wa kuamua yale tunayoyataka na yale tusiyoyataka. Uamuzi ni wako. Jipe moyo na kuamua kuwa mwenye furaha. Jiepushe na hali au mazingira ambayo yatakukosesha amani na furaha. It all begins and ends in your mind. What you give power to has the power over you if you allow it.
 
Msongo wa mawazo kazini ni kitu kinachowasumbua wafanyakazi wengi zaidi na hata wengine hufikia hatua ya kuchukia kazi husika hata kama ina malipo mazuri kutokana na changamoto mbalimbali za kikazi.
 
Hata hivyo, njia sahihi ya kuishi na kuongeza kipato chako ukiwa na furaha ni kujitahidi kufanya kazi na kuepuka njia zinazoweza kukuletea msongo wa mawazo kwa sababu za kikazi, kuliko kutafuta namna ya kuondoa msongo huo. Kinga ni bora kuliko tiba.
 
Hata hivyo, njia sahihi ya kuishi na kuongeza kipato chako ukiwa na furaha ni kujitahidi kufanya kazi na kuepuka njia zinazoweza kukuletea msongo wa mawazo kwa sababu za kikazi, kuliko kutafuta namna ya kuondoa msongo huo. Kinga ni bora kuliko tiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…