Vyanzo vingine vya upoteaji wa madini chuma mwilini ni kupotea kwa damu muda mrefu na kidogo kidogo wakati wa hedhi isiyo na mpangilio, saratani ya mji wa kizazi, malaria sugu, kichocho, bawasili (haemorrhoid), kuharisha damu na vidonda vya tumbo. Mimba za mara kwa mara na kunyonyesha pia hupoteza madini ya chuma mwilini.