Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tuelezee eclipse za jana huko
Maana kuna mwanamke kawa milionea kwa kutengeneza miwani ya eclipse!
Opportunist indeed walahi
Hahahaha
Miwani ilikuwa inauzwa 99 cents - $15 kutegemea na design. Tena kwenye gas stations tu. Amazon huko pia ilikuwepo ya kutupwa. Problem watengenezaji hawakutengeneza mingi. Hapa katikati media wakaanza kupiga debe kuwa total eclipse hii ni ya mwisho kwa kila aliyeko hai kwa sababu nyingine ingetokea baada ya miaka 99. Basi ikawa ni event kubwa ambayo ilikuwa lazima kila mtu aone. Glasses za 99 cents zikaanza kuuzwa 10 bucks na kuendelea. Hoarders na price gaugers wamepiga hela nzuri. Wengine walipoona upungufu wakaanza kutengeneza za kwao feki na kuziuza haraka haraka mtandaoni. Dogo mmoja kapiga $30,000 kwa kuuza basically plastic nyeusi tu akidai ni NASA certified glasses. Waliozinunua na kuzitumia tayari macho yanawauma na moto umeanza kumwakia sijui itakuwaje.

Hizi ni opportunity zinazokuja bila kutegemewa na wenye jicho la ndani ndo wanaweza kuziona.

Pamoja na demands yote hii public library nyingi zilikuwa na stock ya miwani 500 kila moja na anayewahi kabla hazijaisha anapatiwa bure. Mwenyewe nilikwenda kwenye library nikapiga mstari nikapata tena pea mbili. Hakuna kusukumana wala nini.
 
Glaucoma au presha ya macho ni ugonjwa unaoweza kusababisha upofu usipotibiwa kwa wakati.

Tatizo hili linatokea kwenye mshipa wa fahamu ambao husafirisha taswira kutoka kwenye retina ya ubongoni kwa ajili ya kutafsiriwa. Ubongo unapotafsiri taarifa hiyo ndipo mhusika hutambua anachokitazama.
 
Mshipa huo huitwa optiki

Zipo sababu nyingi zinazochangia maradhi haya ila kwa wengi ni kuongezeka kwa presha ndani ya jicho.

Presha hii hutokea baada ya kuongezeka kwa maji ya ndani ya jicho yaitwayo aqueous humour. Maji haya ni maalumu kwa ajili ya kuuelekeza mwanga wenye
 
taswira sehemu ya mbele ya ukuta wa nyuma wa jicho yaani retina na kusafirisha virutubisho na hewa safi kwenye chembehai zilizo ndani ya jicho.

Maji haya hutengenezwa na kutolewa jichoni kupitia mirija iliyopo kwenye ukuta wa mbele wa jicho, cornea na iris.
 
Mirija hii inapoziba, maji haya hujaa jichoni na kusababisha presha au shinikizo liitwalo intraocular pressure likitokea kwa muda mrefu huharibu kuta za optiki hivyo taarifa za taswira kutopelekwa kwenye ubongo kutafsiriwa.
 
Madhara kwenye mishipa ya optiki yakikithiri taarifa kutoka jichoni hazifiki kwenye ubongo hivyo mhusika kushindwa kuona au kutambua akionacho.

Sababu

Mara nyingi si rahisi kufahamu chanzo hasa cha presha ya jicho ingawa inaweza kuwa ni kutokana na kuziba kwa mirija inayotoa maji jichoni au matumizi ya muda mrefu ya aina fulani ya dawa.
 
Kwa ujumla, maumivu makali ya macho au macho kuwa mekundu ni ishara inayohitaji kuchunguzwa. Au ikitokea unashindwa kuona vizuri ghafla au unaona taswira zaidi ya moja na kuhisi kichefuchefu ni dalili za glaucoma.
 
Kwa ujumla, maumivu makali ya macho au macho kuwa mekundu ni ishara inayohitaji kuchunguzwa. Au ikitokea unashindwa kuona vizuri ghafla au unaona taswira zaidi ya moja na kuhisi kichefuchefu ni dalili za glaucoma.
 
Wengine hutapika na kuona rangi zinazofanana na upinde wa jua kuangalia eneo lisilo na kitu huku baadhi wakipoteza uwezo wa kuona vizuri.

Matibabu

Maradhi haya huweza kutibiwa kwa kupunguza presha iliyoongezeka jichoni na madhara yake. Hii hufanywa kwa kutumia dawa za matone pamoja na za aina nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…