Tano, mtu inampasa kuelewa vizuri hisia za wengine, kitu kitakachosaidia kupunguza hasira, na wakati huohuo awe mwepesi kusamehe kwa kuwa ni jambo jema pia kimaisha.
Utafiti uliofanywa mwaka 2001 nchini Uingereza, ulionyesha kuwa mtu anapokuwa na kinyongo fulani kwa mtu, humsababishia kupanda kwa shinikizo la damu pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. Hali hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo, inaweza kuondolewa kwa mtu kuwa mwepesi wa kusamehe haraka.