Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hofu iliyopitiliza huambatana na wasiwasi kupita juu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio yake bila mhusika kuwa na sababu maalum ya kuwa na hofu hiyo.
Watu wenye kuhisi hofu kubwa bila sababu yoyote ya msingi ya kuwafanya wawe hivyo. Mara nyingi watu wenye tatizo hili huhisi janga kubwa litawatokea
 
karibuni au maafa yatawakumba katika maisha yao na daima hawaachi kuwa na hofu juu ya familia zao, fedha, afya, ajira, masomo, au biashara zao.
Maisha yao ya kila siku huwa na mchanganyiko wa hofu, wasiwasi na huzuni, kiasi kwamba hatimaye hofu hutawala mawazo ya mhusika na kuingilia ufanisi wake kazini, kwenye masomo, shughuli za kijamii au uhusiano na mwenza wake.
 
Inakadiriwa watu wazima milioni nne mpaka tano nchini Marekani hukumbwa na tatizo hili kila mwaka. Hapa nchini hakuna takwimu zinaonesha ukubwa wa tatizo hili.
Kwa kawaida, wanawake huathiriwa zaidi kuliko wanaume. Aidha hofu iliyopitiliza mara nyingi huanza kipindi cha utoto mara nyingi kabla ya ujana ingawa inaweza kutokea ukubwani.
 
IMG_3703.JPG
 
Dalili
Hofu isiyo na kikomo huathiri uwezo wa mtu kufikiri ingawa baadaye humletea matatizo ya kiafya. Hali hii inaweza kuambatana na dalili mbalimbali siyo tu zinazohusu kufikiri na akili bali utendaji kazi wa mwili.
Baadhi ya dalili hizo ni kuwa na hisia ya kuwepo kwa janga, kwamba kitu kibaya kitatokea muda wowote na hatari inamnyemelea mhusika.
 
kuhisi kutengwa na ulimwengu, kupoteza hisia, kutojitambua mwenyewe, kuhisi kizunguzungu na kichwa kuuma kuwa chepesi.
Wapo wanaopepesuka wanapotembea au kuwa mvurugo wa hisia, hofu ya kurukwa akili na kupoteza uwezo wa kujidhibiti. Nyingine ni kuhisi kama vile kuna kitu kinachobana kichwani (kama uliyezungushiwa Kamba au rubberband),
 
Back
Top Bottom