Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umbile la Nyumbu (Wild Beast). Nyumbu ana maumbile ya wanyama kadhaa;
1. Miguu ya nyuma na kiuno ni umbile la Fisi;
2. Mkia ni umbile la Farasi
3. Michirizi ya Pundamilia
4. Pembe ni za Nyati
5. Ndevu ni za Pofu
6. Nywele za mgongoni ni za Pundamilia.
7. Nyumbu kwa jina lingine anaitwa "Zero Brain". Hii inatokana na tabia yake ya usahaulifu. Kwa mfano: Nyumbu anaweza kuwa anafukuzwa na Simba, akikuta majani mazuri anajisahau kuwa anafukuzwa anasimama na kuanza kula majani.
Very amazing story!
 
NYUMBU (Wildebeest) ni Mnyama mkubwa anayepatikana Afrika tu katika maeneo ya Savana na kuna aina mbili za nyumbu ambao wana rangi yeusi na mng'ao wa bluu au kahawia. Dume na jike wana pembe zenye umbo la ng'ombe na hupendelea kula majani mafupi.
Nyumbu...Hili neno hili. Haki ya nani naenda jukwaa la siasa sasa hivi. Nitaleta mrejesho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
3fa054aef61aa028b3d72db8b50b0342.jpg
Hahahahaha
 
Mfano Nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba. Kwa wingi wao watafika mtoni na kuanza kunywa maji huku mamba wenye njaa kali wakijikamatia nyumbu mmoja mmoja wakizamisha majini na kujitafunia. Nyumbu waliobaki wataendelea kunywa maji bila kujali yanayowakuta wenzao, wakimaliza kunywa maji wanaondoka zao, lakini wakisikia kiu tena wanarudi palepale bila kukumbuka kuwa kuna wenzao waliotafunwa, na wanaendelea kutafunwa wengine!
 
Nyumbu anatajwa kuwa ni mnyama mwenye uwezo mdogo wa kufikili na katika maisha yake ya kila siku hupenda kujichanganya na wanyama wengine kama pundamilia, nyani wakubwa na baadhi ya ndege wakiwemo yangeyange kama kinga ya kumwezesha kumwepusha au kumshitua na maadui.
Uwezo mdogo wa kufikiri....
 
Maajabu ya Nyumbu hawana utamduni wa kusaidiana pindi mmoja wao anapokamatwa na adui, na wanapofukuzwa na adui kila mmoja hutumia jitihada binafsi za kujiokoa mwenyewe lakini ni mara chache mtoto anaposhambuliwa na wanyama wadogo kimaumbile kama chui ama fisi hupambana naye kuokoa maisha ya mwanaye.
Hawana utamaduni wa kusaidiana...
 
Back
Top Bottom