Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
USHAURI

Punguza ulaji wa nyama nyekundu kama vile nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo na badala yake kula nyama ya kuku. Kula zaidi kuku wa kienyeji na wapike au wachome ili wasiwe na mafuta mengi. Kwa kuku wa kisasa hakikisha hauvunji na kutafuna mifupa yao maana mabaki mengi ya dawa huachwa huko, utakuwa unakula na dawa zilizotumika kuwakuzia na kuwatibia.
 
Sote tunakula mafuta. Na sote tupo katika hatari ya kupata au kuendelea kuwa na matatizo yanayosababishwa na mafuta mengi mwilini. Tunajua kwamba mafuta mengi ni mabaya mwilini na tunapenda kupunguza kula mafuta. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mafuta mengi huleta matatizo na kumuweka mtu katika hatari ya kuwa na unene na uzito mkubwa na uliopitiliza, kupata na shinikizo kubwa la damu, kupata kisukari, kupata magonjwa ya moyo na kadhalika. Yote hayo unaweza kuyaepuka au kusaidia kuyatibu kwa kupunguza mafuta mwilini.
 
JINSI YA KUPUNGUZA ULAJI WA MAFUTA

Njia nzuri zaidi ya kudhibiti mafuta ni kujizuia usile mafuta mengi. Unaweza kufanya hivyo kwa

Kutumia maziwa yaliyopunguzwa au kuondolewa mafuta
Kutumia kiasi kidogo tu cha mafuta katika mapishi
Kuepuka kukaanga vyakula kwa mafuta, na badala yake kutumia njia zingine za kuandaa vyakula kama vile kuchemsha, kuchoma, kuoka, kupika kwa mvuke nk
 
FAIDA ZA KUPUNGUZA MAFUTA

Kupunguza mafuta kutakusaidia kufanikisha mambo yafuatayo

Kukukinga dhidi ya hatari zinazoletwa na mrundikano wa mafuta mengi mwilini
Hatari za mrundikano wa mafuta mengi mwilini ni pamoja na kuganda kwenye mishipa ya damu na moyo na kupelekea kupungua kwa njia ya kupita damu na moyo kutumia nguvu nyingi sana kusukuma damu. Hatima yake ni magonjwa ya moyo, presha na magonjwa mengine ya mishipa ya damu.
 
U2. Kudhibiti Uzito mkubwa na Magonjwa yanayosababishwa na Mafuta mengi mwilini

Kupunguza mafuta husaidia sana kudhibiti matatizo mbalimbali kama vile uzito mkubwa na unene uliopitiliza, kisukari, presha, matatizo ya moyo nk. Ni muhimu sana kwa watu wote ambao wanaendelea na matibabu kujitahidi sana katika suala hili na kupima maendeleo yao mara kwa mara. Husaidia wagonjwa kupata afadhali, husaidia kuongeza ufanisi wa dawa na matokeo mazuri kuonekana haraka.
 
WAFAHAMU WANYAMA WANAOCHANJA MBUGA (MBIO)
Leo nimeona si mbaya kama nitakuletea habari ya viumbe hai ambao wanaspidi kubwa huko hifadhini, ili siku ukijichanganya ukaingia kwenye kumi na nane zao, yakitokea yakutokea ujue unakimbizwa na nani na uwezo wake kukimbia ukoje, kama nilivyo huwa nakuletea mambo live kutoka mbuga zetu tuu yaani Serengeti, mikumi, ngorongoro, katavi, kutulo, ruaha nk, hivyo sitegemei utamuona mnyama kama kangaroo au wolf japokuwa nao ni kiboko katika mbio lakini kwa bahati mbaya hapa kwetu hao jamaa hawapo kabisa, baada ya utangulizi huo naomba sasa nianze na list yangu.
 
Chui
Moja kati ya viumbe niliowahi kuwachambua kama utatizama katika ukurasa huu ni chui, nilikueleza sifa yake kubwa huyu kiumbe ni kwamba ana aibu sana, hamuwezi tizamana usoni na ukilazimisha jambo hilo basi yeye huwa anajifanya eti kalala usingizi, nilikueleza pia ni mjanja mjanja na muongo, ukitaka kujua hilo sikia hii, anapokuwa na njaa aibu zake huweka kando kwani mbuga nzima yeye ndio bigwa wa riadhaa ana uwezo wa kukimbia 120 km kwa kutumia saa moja tuu.
 
Swala.
Mnyama pekee anayeishi pasina amani sababu ya unyonge wake, swala hata sungura akipita katikati ya miguu yake yeye huwa anaruka juu, kwakuwa anajua tayari kumekucha, hupendelea kukaa jilani na wanyama wababe kwa sababu ya usalama wake mfano tembo, twiga na nyati, pamoja na unyonge wake lakini mbio tuu alipewa, anaweza kimbia kwa spidi moja na chui na wakati mwingine akamshinda lakini chui akimkomalia atamkamataa tuu kwakuwa kenyewe huwai kuchoka, anauwezo wa kukimbia km 88 kwa saa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…