Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-09-24-14-48-53.png
 
Lilikuwa ni gari kubwa la kusafirisha mafuta ndani na nje ya nchi huku limefunga matela mawili na kukatiza barabara, lakini kwa sababu ya udogo wa barabara, wingi wa watu pamoja na bodaboda vilimpa wakati mgumu dereva na kulazima kupiga honi ili kuwatawanya watu.

Wakati nikiendelea kuangalia lile lori niligudua dereva aliyekuwa akiendesha alikuwa mwanamke. Nilizidi kuvutiwa na ujasiri wake
 
kwani alionekana wazi kuwa hakuwa na woga kabisa jambo lililosababisha sehemu kubwa ya watu waliokuwepo eneo lile kupigwa butwaa.

Haijazoeleka kwa Watazania wengi kuona mwanamke kama huyo akiendesha lori lenye tela nyuma kwani wengi wanaamini kazi ngumu zimekuwa zikifanywa na wanaume.
 
Kulingana na imani na tamaduni za Waafrika wengi, mwanamke ni kiumbe dhaifu na hupaswa kukaa nyumbani kusubiri kuletewa na mume wake mahitaji yote huku yeye akiendelea shughuli za nyumbani zikiwemo, usafi na kuandaa chakula na kutunza familia na hata anapolazimika kufanya kazi basi ni zile nyepesi na si za shuruba.
 
Kulingana na mfumo dume uliopo wengi huamini kuwa mwanaume ndiye anayeweza kufanya kazi ngumu kama hizo, hivyo kwa tukio la kumwona mwanamke huyo akiendesha lori lile ilisababisha wengi kuduwaa na kukosa majibu.

Tukio hilo lilinivutia na kuamua kuachana na shughuli zangu nyingine na kumfuatilia mwanamama huyo ambaye alionekana wazi kuipenda kazi yake.
 
Kwangu naweza sema ni bahati ya mtende, kwani mwanamama yule baada ya kukata kona alikwenda moja kwa moja kuegesha gari yake katika kituo cha mafuta kilichopo mita chache na zilipo ofisi za gazeti hili na kunipa nafasi ya kumfuata ili kuzungumza naye kwa undanikuhusu kazi yake.
 
Kazi ya ndani yamleta jijini Dar

Baada kuzungumza naye anasema anaitwa Happy Swaga, mkazi wa mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Happy, alimaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Mvumi, Makulu mkoani humo mwaka 1998.

Anasema mwaka 2000 aliletwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani maarufu kama ‘house girl’.
 
Tangu nilipokuwa mdogo wakati nasomoa mawazo yangu yalikuwa ni kuwa dereva na kazi nyingine niliyoipenda ilikuwa ni askari jeshi lakini baada ya kumaliza darasa la saba sikufaulu nikawa mtu wa nyumbani kumsaidia mama mpaka pale nlipopata safari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani.

“Nilifanya kazi hiyo kama miaka mwili mpaka pale bosi wangu alipofariki na nikaona kuna haja ya kutafuta njia nyingine ya kujiingizia kipato kwani umri wangu ulikuwa umesogea.”
 
Anasema alitafuta kazi hotelini na kupata ingawa hakuifanya kwa muda mrefu kutokana na mazingira yake kutoyapenda huku kipato kilikuwa kidogo sana.

“Baada ya kuacha nilibahatika kupata kazi ya kuuza vinywaji katika baa moja maarufu jijini Dar es Salaam, lakini niikutana na changamoto kubwa na kuamua kuachana na kazi hiyo,” anasema Happy ambaye ni mama wa watoto wawili wa kike, Mariam (16) ambaye anasoma kidato cha nne na Josephine (13) kidato cha kwanza.
 
Back
Top Bottom