Ninapopakia mzigo bandarini, siondoki siku hiyo na safari huwa naianza asubuhi alfajiri kama ni Zambia, kituo changu cha kwanza huwa ni Mafinga kwa mwendo wa kawaida huwa naingia hapo saa mbili usiku na kulala hapo hapo.
“Saa 12 alfajiri naanza safari hadi saa 10 jioni naingia mpakani Tunduma kituo changu cha pili, kunapokucha nahangaikia kupata vibali vya kuvuka ng’ambo na siku hiyo inakuwa ya tatu na siku ya nne navuka naingia Zambia,” anasena Happy na kufafanua kero yake hapo mpakani ni kuchukua muda mwingi kuvuka huku foleni inachukua hadi saa sita.
Uhusiano wake wa kimapenzi
Ukimtazama Happy katika kidole chake cha pili cha mkono wa kuume, amevaa pete ya ndoa na anafafanua: “Hii pete ndugu yangu naivaa kujifariji tu na nisisumbuliwe barabarani mimi msela, natamani kuolewa ila bado sijapata mchumba.”