Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ila jaman dini zinachizisha watu
Hivi kale kachungaji feki leo kameshaonekana hapa?
72033ea046675002adf2c7e90e5701e7.jpg
 
Afya ya nyayo

Si jambo geni kumuona mtu akihangaika kujisugua nyayo anapooga au anapotawadha.Kwa maeneo ya mjini, hivi sasa wapo vijana waliojiajiri wakitumia zana za kisasa kusugua visigino vya kina dada ili ving”ae.

Kwa nini watu wanasafisha nyayo? Wanafanya hivi ili kukabiliana na tatizo la afya ya nyayo ikiwamo nyayo kupasuka kwa ngozi au kutengeneza vidonda.
 
Matatizo mengine ya kiafya yanayoweza kuzikumba nyayo ni pamoja na sunzua za nyayoni (wats) hili ni tatizo linalotokea kwa uchache linasababishwa na maambukizi ya virusi vya Papilloma.

Fangasi za nyayoni ambazo mara nyingi huwapata watu wanaishi maeneo yenye joto, husababisha nyayo hasa katika ya vidole kulika na kupukutika na kuwa na mwasho mkali.
 
Matatizo mengine ni pamoja na kupata maumivu katika nyayo, yanaweza kuwapo katika kisigino au mbele kabla ya vidole mara; nyingi unaweza usikute jeraha lakini maumivu yakawepo.

Wanawake ndio waathirika zaidi ya maumivu ya unyayo hasa maeneo ya kisigino, hii ni kutokana na hulka ya kuvaa viatu virefu na kubadili viatu vyenye urefu wa kisigino tofauti tofauti.

Endapo muathirika atakua akihisi maumivu makali ya kuchoma, huenda tatizo ni kukandamizwa na kujeruhiwa kwa mishipa midogo ya fahamu.

Mara nyingine kama ni maumivu ya kawaida huenda yakawa ni shambulizi la tishu lililojitandika ndani ya nyayo.
 
Nyayo inaweza kupata uvamizi wa funza ambao huweza kujihifadhi humo na kuzaliana, husababisha mwasho, kukereketa na maumivu.

Watu wa maeneo ya mashambani yenye panya kwa wingi hukutana na matatizo ya nyayo, kutokana na wanyama hao nyakati za usiku kupendelea kutafuna eneo la nyayoni.

Tatizo la magaga

Magaga au wengine huita sagamba ni hali ya nyayo kuwa na ganda gumu lenye tabia ya kupasuka pasuka. Ni tatizo ambalo kina dada wengi hawapendi kuwa nalo hasa kutokana sababu za kiurembo.

Kupasuka kwa nyayo na ganda la nyayo kuwa kubwa kupita kiasi, kuna sababishwa na dosari ya kimwili kurundika tishu ya nyayo kupita kiwango cha kawaida.
 
Kuwepo kwa hali ya ukavu na kukamaa kwa nyayo na kuendelea kupata shinikizo la uzito wa mwili, husababisha hali hii ambayo baadaye inaweza kumfanya mhusika kupatwa na vidonda vinavyoambatana na maumivu sehemu ya ndani ya nyayo.

Tiba ya nyayo zinazopasuka

Moja ya matibabu rahisi ya kuepukana na kupasuka kwa nyayo ni kuimarisha usafi wa mwili kwa jumla; unaweza ukaloweka miguu yako katika maji ya uvuguvugu yenye sabuni kwa muda wa dakika 10 hadi 15.

Fanya hivyo asubuhi na jioni kila unapotaka kuoga, tafuta kifaa safi chenye uwezo wa kusugua pasipo kuleta majeraha.
 
Back
Top Bottom