Nyayo inaweza kupata uvamizi wa funza ambao huweza kujihifadhi humo na kuzaliana, husababisha mwasho, kukereketa na maumivu.
Watu wa maeneo ya mashambani yenye panya kwa wingi hukutana na matatizo ya nyayo, kutokana na wanyama hao nyakati za usiku kupendelea kutafuna eneo la nyayoni.
Tatizo la magaga
Magaga au wengine huita sagamba ni hali ya nyayo kuwa na ganda gumu lenye tabia ya kupasuka pasuka. Ni tatizo ambalo kina dada wengi hawapendi kuwa nalo hasa kutokana sababu za kiurembo.
Kupasuka kwa nyayo na ganda la nyayo kuwa kubwa kupita kiasi, kuna sababishwa na dosari ya kimwili kurundika tishu ya nyayo kupita kiwango cha kawaida.