Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kwa kuwa vitu hivi vipo katika kiwango kidogo kwenye damu hali hii itapelekea ubongo nao usiwe na sukari na Oksjeni ya kutosha hivyo kutofanya kazi yake sawa sawa. 3.Kuwa na shinikizo la chini la damu. 4.Kuwa na maambukizi mwili kama yatokanayo na vimelea vya bacteria (SEPCEMIA),au Fangasi (Cryptococcal),Virusi hasa HIV wanapoingia kwenye ubongo. 5.Kuwa na homa kali itokanayo na Malaria au Uti wa mgongo(Meningitis). Hii ndiyo degedege kwa ufupi degedege ni dalili ya ugonjwa usiojulikana kwani inaweza kuwa ni matokeo ya kuwepo kwa mojawapo ya magonjwa tuliyataja hapo juu.