Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dalili na ishara za Pumu ya papo, huwa na dalili na ishara hatari kama mapigo ya moyo kwenda mbio, kupumua kwa shida, kutoa sauti kama miluzi, kukooa sana na kifua kubana sana, wai hospitali ili kupata huduma mapema ili kuepuka kifo kitakachosababishwa na kuongezeka kwa hewa ya Carbondioxide katika damu na upungufu wa oxygen na hivyo kuharibu ubongo na mfumo wa upumuaji.
 
Dalili na ishara za shambulio la moyo, kama maumivu makali ya kifua, mikono, shingo na taya, uchovu mwingi, kichefuchefu, kutapika, kukosa nguvu, na kutokwa na jasho kali kipindi cha baridi.Upatapo dalili hizi wasiliana na wataalamu wa afya mapema watakaokuelekeza dawa kwa ajili ya kulinda na kurekebisha mapigo ya moyo na kulinda mishipa na misuli ya moyo.
 
Dalili na ishara za mtu kujinyonga, usipuuze unapoona dalili hizi ni hatari sana kama msongo wa mawazo, uchungu, huzuni, masikitiko, uchovu wa muda mrefu, kutojali, wasi wasi, kukosa usingizi na hamu ya kula na kujifikiria vibaya.Unapaswa kuwasiliana na madaktari au wataalamu wa saikolojia au ndugu wa karibu.
 
Miaka mitatu iliyopita mpwa wangu 22 yrs old aliumwa na mbwa. Tukamwambia kwenda kupata sindano jamaa mshua mbishi sana kizazi cha dot com full mlegezo na ujeuri. Baada ya wiki kama mbili hivi mwili ukaanza kumuwasha. Hatujakaa sawa akaanza kuongea maneno yasiyoeleweka non stop. Tukampeleka hospitali sasa kawa kama kichaa kabisa madaktari (bila kufanya vipimo) wakasema huyu mpelekeni kwa waganga kwa sababu hana Malaria wala nini. Nikawaambia kuwa 2-3 weeks ago aliumwa na mbwa. Madaktari hawakunisikiliza. Tukampeleka hospitali nyingine ya binafsi ndiyo wakathibitisha kuwa ni rabies, na kwamba hakukuwa na tiba. Yaani kijana mpaka anakata kauli alikuwa anazungumza kama cherehani. Mpaka leo huwa niko guilty kwamba pengine ningefanya kila liwezekanalo hata kama ni kumuitia polisi ili kuhakikisha kuwa anatapata hizo sindano kwa nguvu angepona. Apumzike kwa amani !

Kitu kingine: Baada ya kufariki mwili wake ulianza kuvimba. Mkanganyiko hapa ukatokea na imani za kishirikina zikaingizwa. Kwa uzoefu wako, ni kawaida kwa mgonjwa aliyefariki kwa rabies mwili wake kuvimba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…