Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ATHARI ZA MVINYO KWA AFYA YAKO.

Pamoja na kutumiwa kupunguza uchovu, kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kuharisha, kutapika na kuzuia maumivu watafiti wanadai kuwa mvinyo mwekundu (Red wine) hauna manufaa kama ilivyodhaniwa kuwa nayo kwa moyo wa binadamu pale unapotumiwa mara kwa mara na kupita kiasi kama ifuatavyo.
 
Kudhoofisha mifupa, utumiaji wa pombe muda mrefu usababisha kudhoofika na kuvunjika kwa mifupa kwa kuathiri cell ambazo hutengeneza mifupa.
Kansa, hutumiaji wa wine kupita kiasi au kwa muda mrefu husababisha hatari ya kupata saratani ya koo, tumbo, utumbo, mapafu na maziwa,
 
Kuhathiri mfumo wa damu, utafiti unaonyesha kuwa unywaji wa mvinyo kupita kiasi husababisha magonjwa ya moyo, mishipa na damu kwa kubadili mapigo ya moyo na kupunguza kolesteroli ambazo hurekebisha mzunguko wa damu
Matatizo ya akili, hutumiaji wa wine kwa muda mrefu uharibu uwezo wa akili asa katika tabia, kumbukumbu na uwezo wa kutambua vitu kwa kuharibu seli katika ubongo.
 
Ugonjwa wa kisukari, unywaji wa pombe kupita kiasi usababisha kuongezeka kwa sukari mwilini wakati unywaji wa kawaida hupunguza uwezekano wa kupata kisukari.
Maumivu ya kichwa, hii hutokana na kupoteza maji mengi na kemikali zilizo katika mvinyo kama histamine, serotonini kama inavyoonekana katika hangover.
 
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
 
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
Kushindwa kupumua vizuri
Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
Sehemu nyeupe ya jcho kuwa bluu
 
1507142846327.jpg
 
Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
Kucha kuwa dhaifu
Kusikia hasira na kuhamasika haraka
Kuchoka sana kuliko kawaida
Maumivu makali ya kichwa
Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
Uchovu wa mara kwa mara
 
MATIBABU

Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali ambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
 
DAWA ZA NYWELE ZINAVYOSABABISHA UVIMBE KATIKA KIZAZI

Dawa za kulinisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.
 
Pia dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.
Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids mara nyingi kabla mwanamke hajaacha kuzaa.
 
Baadhi ya dawa za nywele husababisha matatizo ya upumuaji, tumbo, kuunguza fuvu, nywele kukatika na kunyonyoka au kupoteza nywele moja kwa moja hivyo inakupasa kupata ushauri au kusoma maelekezo kabla ya kuchagua aina bora ya dawa kutokana na nywele zako.
 
TATIZO LA KIKOHOZI CHA MUDA MREFU.

Kukoa ni kitendo cha kuondoa uchafu au kamasi ili kusafisha njia ya juu ya hewa. Kikohozi cha muda mrefu ni kikohozi kisichopona kwa zaidi ya wiki 3 2 na kuendelea na huwa sio ugonjwa bali ni ishara ya ugonjwa au tatizo lililopo mwilini kama ifuatavyo:
 
Uvutaji wa Sigara, kwa kawaida wagonjwa wengi wa kikohozi cha muda mrefu huwa ni wavutaji wa sigara na baadhi hupona pale wanapoacha na wengine huchelewa baada ya kuwa wamepata matatizo mengine makubwa katika njia ya hewa.
 
Back
Top Bottom