Kwa mwanaume wa kawaida kiwango hicho kinaweza kuwa kati milioni 35 mpaka milioni 200. Hii inasababisha kuwepo kwa wastani wa manii milioni 400 kwa kila mililita kazaa kwa kila tendo.
Ikiwa kiwango hicho kitapungua na kuwa chini ya milioni 20 mwanaume hatakua na uwezo wa kuzalisha. Uwezo wake wa kuishi ndani ya joto la kawaida la binadamu ni masaa 24 mpaka 48.
Zinaitaji joto nyuzi 2 sentigredi ili kuweza kuzalishwa. Na hii ndo sababu hasa ya korodani kukaa kwenye mifuko yake(scrotum) nje ya mwili ili kupata joto 2 nyuzi za sentigredi kuweza kuzalisha manii.
Watu wengi wamezoea kusikia na kushuhudia madhara tofautitofauti yanayosababishwa na unywaji pombe kupita kiasi. Pombe imesabisha madhara mengi hasa katika jamii zetu za nchi zinazoendelea.
Lakini kwa wakati mwingine kutokana utafiti uliokwisha kufanywa na wanasayansi mbalimbali inaonesha kuwa endapo pombe itatumika ipasavyo kwa kiwango stahiki inamchango katika afya ya mwili wako.
Kutokana na utafiti uliofanya huko amerika inashauriwa kwa mwanamke kunywa bia moja kwa siku na bia mbili kwa mwanaume kwa siku. Hicho ndo kiwango cha unywaji wa kawaida na sio kupitiliza.
1. hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
2. Hupunguza hatari ya kupata stroke.
3. Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kisukari.
4. Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya akili.
5. Husaidia kukupa kinga zidi ya mafua ya kawaida.
6. Huongeza hamu ya kufanya mapenzi.
1. Figo hutoa taka mwili na kemikali nyingine ambazo hazina kazi mwilini zitokanazo na vyakula.
2. Figo inaweka sawa uwiano kati ya maji na madini chumvi ndani ya mwili.
3. Figo inarekebisha kiwango cha madini chumvi yapatikanayo ndani ya mwili.
4. Figo inasaidia kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.
5. Figo huzalisha homoni ndani ya mwili nkama vile renin
6. Figo uzalisha glucose kutoka kwenye vyanzo vingine mwilini kama vile protein na fat wakati mwili umepungukiwa na glucose.
Ni moja kati ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na vrusi viitwavyo Human papilloma virus(HPV).Ugonjwa huu unaweza kusambaa kwa kufanya ngono ukeni, mdomoni na hata pia kufanya ngono kinyume na maumbile. Husambaa kwa kasi kubwa kwa kufanya ngono ukeni na kufanya ngono kinyume na maumbile.
Pia HPV unaweza kuupata hata kama uliyefanya nae ngono hakuonesha dalili zozote za ugonjwa huon. Ni vigumu kwa mtu aliyeupata ugonjwa huu kwa mara ya kwanza kuutabua kwasababu ugonjwa uaweza kujitokeza baada ya mwaka mmoja.
HPV husababisha matatizo ya kiafya kama vile vipele sehemu za siri.
Ugonjwa huu hauna tiba ila chanjo yake inapatikana.
Chanjo hiyo ya HPV mpaka sasa inapatikana hapa nchini.
Kwa vijana wote wa kike na wakiume waliopo kati ya umri wa miaka 11 au 12 wanaweza kupata chanjo hiyo.
Pia inashauriwa kwa wanaume katika umri wa miaka 21 na kwa wanawake katika umri wa miaka 26 kupata chanjo ya hpv kama hawakupata pindi wakiwa wadogo.
Kinga hiyo ya hpv pia inashauriwa kupewa wanaume au wanawake wenye kinga isiyo imara kupambana na magonjwa kama vile watu wenye VVU au UKIMWI wenye umri kati ya miaka 26 kama hawakupata chanjo hiyo pindi wakiwa wadogo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.