Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1507396140255.jpg
 
Kama umekata tamaa, nakutia moyo uendelee mbele, kukata tamaa ni kujiumiza. Ulishaanza kwa nini ukate tamaa? Badili mbinu na endelea mbele. Kama unaendelea mbele hongera sana, maana mafanikio ni safari hayaji ghafula tu. Endelea kupigana kila siku kwa kuweka juhudi na kujifunza kutokana na makosa na husikate tamaa.
 
Leo tunaenda kujifunza faida ya kusema ukweli katika safari yako ya mafanikio. Mambo yamebadilika siku hizi, kuwa mkweli imeonekana ni ushamba. Ukiwa mkweli unakuwa kama mwiba kwa watu wengine. Na watu wengine wanaweza kukuchukia kabisa kwa sababu tu unasema ukweli. Watu wengi sio waaminifu siku hizi, kila mtu anavutia upande wake.
 
Mtu yuko tayari kusema uongo apate pesa. Mtu yuko tayari kudanganya ili apate kazi. Mtu yuko tayari kudanganya ili hasioenekane mshamba. Dunia imebadilika sana siku hizi, kusema ukweli imeonekana kama ni ujinga. Watu wakweli kwenye Dunia ya sasa ni wachache sana, kwa sababu mazingira yanatuaminisha kudanganya ndo habari ya mjini. Mazingira yanatuaminisha,
 
ukiwa mkweli huwezi kufanikiwa. Mimi nimeshuhudia mtu yuko tayari kusema baba yake au mama yake amekufa kwa sababu tu anataka afanikiwe. Rafiki kusema uongo ndo habari ya mjini siku hizi. Ukiwa mkweli basi unaonekana mshamba.
 
Rafiki kuna watu wengi wamepoteza kazi zao kwa sababu wameonekana waligushi vyeti vyao. Walijiona wajanja mwanzoni lakini sasa ndo wanaonekana washamba. Kuna watu wamepoteza wateja katika biashara, kwa sababu waliwaahidi jambo na wakashindwa kutekeleza
 
Back
Top Bottom