Unapokosea, itakubidi upate muda wa kufanya tena au kutatua kosa ulilolifanya kabla ya kupata kile ulicholenga. Hivyo kwa njia hii tunaweza kujifunza kuwa na subira na uvumilivu.
Mara nyingi tunakosea kutokana na kushindwa kutumia pesa vyema. Tunapokuwa kwenye matatizo kutokana na makosa ya matumizi mabaya ya pesa; tutajifunza kuwa wakati mwingine inatupasa kutumia pesa vyema.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kujiwekea malengo vyema maishani. Lakini tunapokwama, moja kwa moja tunajifunza jinsi ya kuyabadili au kuyaboresha vyema wakati mwingine.
Ikiwa utafanya kosa kutokana na aina ya marafiki ulio nao, ni wazi kuwa kosa hilo litakufundisha umuhimu wakutazama aina za watu au marafiki unaoshirikiana nao. Marafiki bora watakutia moyo na kukuhamasisha kuendelea mbele ili kutimiza malengo yako na siyo kukuzamisha.
Naamini umefahamu kuwa makosa ni shule nzuri ikiwa tutaweza kutulia na kupata kile tunachofundishwa. Moja ya tabia ya watu waliofanikiwa na werevu ni kujifunza kutokana na makosa yao.
Mambo yote katika maisha yetu yamefungwa kwenye muda, hivyo ni vyema kufahamu namna bora ya kutumia muda kwa njia yenye mafanikio.
Kutumia muda vyema siyo tu kutakuwezesha kufanya kazi vyema, bali kutakuwezesha kuishi maisha vyema. Ni muhimu kupata muda wa kufanya mambo yote ya muhimu kwenye maisha yako, kwani kila moja lina nafasi na umuhimu wake.
Hapa nitaeleza kanuni 9 yatakayokuwezesha kutawala muda vyema.
1. Anza na panga siku yako vyema
Usikimbilie kuanza majuku yako ya siku bila kukaa chini na kutumia dakika chache za kutafakari mambo kadhaa.
Tafakari ni jambo gani muhimu zaidi ili uweze kulipa kipaumbele katika siku yako.
Jifunze kujiwekea malengo, haya yatakuwezesha kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku yako. Kwa njia hii utaweza kukamilisha vitu kulingana na muda uliojiwekea.
Usifanye kila kazi kwa kuwa unaweza kuifanya. Kama una mtu au watu ambao unaweza kuwagawia majukumu fanya hivyo, kwani kwa njia hii kazi nyingi zitafanyika ndani ya muda mfupi.
Bainisha kazi zinazoweza kufanywa na wengine, andaa muongozo wa kuzifanya kisha acha watu wengine wazifanye.