Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kawaida binadamu anahitaji saa 7 hadi 8 za kulala. Hivyo hakikisha unapata muda huu hadi muda ule unaotaka kuamka. Kwa mfano, ikiwa unataka kuamka saa 11 asubuhi, unatakiwa kulala saa 3 au 4 usiku. Kwa kufanya hivi mwili wako utapata muda wa kutosha wa kulala na kukuruhusu kuamka mapema asubuhi.
 
Lala katika mazingira sahihi

Siyo mazingira yote yanayofaa kwa binadamu kulala. Mazingira mengine humfanya binadamu kuwa mchovu na kutopata usingizi mzuri. Ili kuhakikisha umepata usingizi mzuri na wa kutosha, hakikisha mazingira unayolala ni rafiki. Unaweza kufanya haya yafuatayo:
 
Hakikisha chumba unacholala kina hewa ya kutosha.
Hakikisha unatumia mto na godoro bora.
Ondoa kelele na usumbufu mwingine katika eneo unalolala.
Zima taa au tumia mwanga hafifu wakati wa kulala.
Tawala joto la chumba unacholala.
Kwa kuzingatia haya utapata usingizi wa uhakika na wakutosha; hivyo utaweza kuamka mapema asubuhi ukiwa na nguvu na afya.
 
Hakikisha chumba unacholala kina hewa ya kutosha.
Hakikisha unatumia mto na godoro bora.
Ondoa kelele na usumbufu mwingine katika eneo unalolala.
Zima taa au tumia mwanga hafifu wakati wa kulala.
Tawala joto la chumba unacholala.
Kwa kuzingatia haya utapata usingizi wa uhakika na wakutosha; hivyo utaweza kuamka mapema asubuhi ukiwa na nguvu na afya.
 
Tengeneza ratiba ya kulala inayoeleweka

Kutokana na shughuli nyingi au mtindo fulani wa maisha, watu wengi hawana ratiba inayoeleweka ya kulala.

Utamkuta mtu leo analala saa nne, kesho saa tatu, keshokutwa saa sita, siku nyingine saa mbili n.k. Jambo hili hukufanya kuwa na mfumo duni wa kulala na kutopata usingizi bora; kumbuka usipolala vizuri hutoweza kuamka vyema mapema asubuhi.

Jiwekee ratiba nzuri ya kulala na kuamka leo na uifuate.
 
Epuka vitu vinavyovuruga usingizi

Vipo vitu na tabia mbalimbali zinazoweza kuvuruga usingizi wako na kukufanya kushindwa kuamka kwa wakati asubuhi. Matumizi ya vitu kama vile caffeine, ulaji wa vyakula vizito usiku au matumizi ya vifaa vya kielektroniki huweza kuvuruga usingizi wako kwa kiasi kikubwa.

Hakikisha vitu unavyovitumia au kuvifanya jioni ama usiku, havivurugi ubora wa usingizi wako.
 
Weka malengo

“Jiwekee lengo litakalokufanya uruke kutoka kitandani asubuhi”
The Color Run
Ni lazima ujiwekee lengo la kwanini uamke asubuhi; ni lazima pia ufahamu manufaa ya kuamka asubuhi. Hakikisha unajiwekea lengo na unafanya bidii kulitimiza.
 
Ikiwa unataka kutumia alamu kama njia ya kukuamsha basi iweke mbali na kitanda chako; kwa kufanya hivi itakubidi uamke ili uende ukaizime.

Hili litakusaidia sana kwani utakuwa tayari umeshatoka kitandani; hivyo usirudi tena kitandani na endelea na ratiba nyingine ulizojiwekea asubuhi.
 
Usikubali kudanganywa na akili

“Nitaamka tuu baadaya ya muda kidogo”, “Kwanza kuna baridi”, “Nitawahi sana”, “Sitachelewa”, “Nitafanya haraka”, “Mambo mengi nilifanya jana” n.k. ni baadhi tu ya kauli ambazo watu wengi hudanganywa na akili zao ili walale zaidi.
 
Usikubali kushawishiwa na mawazo haya; mara muda wa kuamka ufikapo, amka kweli na usiendelee kulala tena. Njia hii itakuwezesha kuamka bila kujishauri na kuruhusu akili kukudanganya.

“Unatakiwa kuwa na ndoto ili uweze kuamka asubuhi”
Billy Wilder
 
Mwombe mtu akuamshe

Hii ni moja kati ya njia bora sana za kuamka asubuhi kama utapata mtu sahihi. Ikiwa kuna mtu anayeamka mapema kuliko wewe au anayeamka wakati unapotaka kuamka, basi mwombe akuamshe.
 
Badili ratiba ya kuamka

Njia hii ya kubadili ratiba ya kuamka inaweza kukusaidia kuamka kwa wakati ikiwa utafanya muda wa kuamka uwe mapema zaidi. Kwa mfano ikiwa unataka kuamka saa 11:30 asubuhi, basi jitahidi kuamka saa 11:00 asubuhi.

Kwa kufanya hivi utaufundisha mwili wako kuamka mapema hata kabla ya muda ule uliopanga kufika; hivyo hutahitaji kujilazimisha kuamka wakati wa kuamka utakapofika.
 
Panga ratiba ngumu asubuhi

“Kama unataka kufanya ndoto zako zitimie, jambo la kwanza ni kuamka”
JM Power
Njiaa hii ya kupanga ratiba ngumu asubuhi itakuwezesha kukuhamasisha na kukuhimiza kuamka mapema na kwa wakati. Hii ni kutokana na sababu kuwa huna muda mwingine wa kutekeleza ratiba husika kwani zinahitajika zitekelezwe asubuhi.

Hakikisha majukumu yako mengi unayapanga kwenye muda wa asubuhi; ikiwa kuna mtu unayetakiwa kukutana naye, pia panga mkutane asubuhi.

Hakikisha unajiwekea ratiba, tena hakikisha ratiba yako inaanza mapema kabisa na unaizingatia.
 
KISA CHA MFALME NA MCHAMUNGU. Kwa wasomaji wapya. Mfalme BWANGA alisifika kwa mbwembwe na majivuno kwenye Taifa lake. Siku moja Alihitilafiana kidogo na mchamungu masikini, pale alipoambiwa kuwa MOLA muumba Mbingu na nchi ana uwezo wa kugeuza maisha yake yakawa dhalili na kuwanyanyua walio dhalili kwa uweza wake. Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mfalme huyo. Siku moja baada ya ushawishi mkali akiwa na jopo la wapambe na walinzi wake alifanikiwa kumnunua farasi mzuri wa ajabu aliyeonekana kiajabu sokoni. Alipompanda ili ajaribu kumuendesha akarushwa naye na kudondoshwa msituni mbali kabisa na himaya yake. ENDELEA. Wakati Mfalme Bwanga akitaharuki na kushangaa tukio la kurushwa na kudondoshwa kwenye msitu asioujua akiwa bila mlinzi hata mmoja. Mfalme akiwa kwenye kushangaa, farasi aliruka tena mwenyewe, akamdondosha chini na kumuacha mfalme pekekee kwenye msitu huo mnene. fumba na kufumbua Mfalme akajikuta mpweke kwenye mahali pa kutisha bila ya msaada wa binadamu yeyote. himaya yake, mali zake, walinzi wake vyote havikuwa na msaada wala thamani kwa muda huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…