KISA CHA MFALME NA MCHAMUNGU...... Kulipopambazuka Mfalme akaweka nia, kwamba mchana huo apambane mpaka afike kwake. Na pia akawa na matumaini makubwa kuwa huko nyumbani familia yake, walinzi na raia wake wanamtafuta. Mfalme alitembea kwa morali. mchana ulipoingia mfalme alikuwa na njaa kali na kiu, asijue mahali pa kupata japo mihogo ya kuchoma, mahindi ya kuchoma kwa ndimu, achilia mbali chakula kizuri kwenye jumba la kifalme. Mfalme baada ya kufikiria kwa muda ikabidi atafute matunda ya porini ili apoze njaa. Na baadaye changamoto kubwa kwake ikawa mahali pa kupata maji ya kupoza kiu yake.