MFALME BWANGA. Mfalme alibaki kwenye hali hiyo akiwa porini kwa miezi minne. Mwezi wa tano, asubuhi moja akaona nyumba akajisogeza, kabla hajaomba maji wala chakula akajitambulisha kuwa yeye ni mfalme, akidhani yupo kwenye nchi yake. Mwenyeji aliyekutana naye akashangaa, mfalme gani ana manywele, madevu marefu na machafu, amevaa nguo zilizolaruka. (ieleweke kuwa muda aliokaa mfalme porini hakupata zana ya kunyolea nywele na ndevu na hata hivyo hicho haki kuwa kipaumbele chake, kipaumbele chake ilikuwa kufika nyumbani. pia kutokana kukwaruzwa na miti nguo zake zililaruka) mwenyeji yule akaona huenda ni mwendawazimu anampa majaribu. Yule jamaa akaingia ndani akatoka na bakora akamcharaza, MFALME wetu akakimbilia tena msituni kujiokoa
INAENDELEA....