Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KISA CHA MFALME NA MCHAMUNGU.. MFALME baada ya kucharazwa bakora akakimbilia msituni. Kitendo cha kucharazwa mikwaju kikamfanya awe na tahadhali. Hivyo baada ya kukwepa kipigo akatembea kando kando ya kijiji kile, jioni akajipeleka kwenye nyumba nyingine. Alipofika akatoa salaam kwa upole kisha akaomba maji ya kunywa, baadaye akajieleza kuwa yeye ni msafiri aliyepotea ambaye anautafuta mji wa mfalme Bwanga . mtu huyu alimuhurumia, akampa chakula kisha akamuonyesha njia ya kuelekea mji wa mfalme Bwanga .baada ya kutembea usiku mzima alfajiri akafika kwenye kasri lake la kifalme. Akagonga mlango kwa Vishindo. Mlinzi alipokuja akakuta mtu mchafu, aliyevaa matambara, asiye na viatu, mwenye madevu na manywele makubwa, machafu na yaliyotimka. Askari akamuuliza shida yake. Mfalme akajitambulisha kwa mbwembwe na amri za kifalme, "Fungua mlango mimi ni mfalme" mlinzi akauliza "nani, wewe ni mfalme"? Akamuingiza ndani kisha akamuweka kwenye rumande ya pale getini. Mlinzi akaingia ndani ya kasri akaenda kumueleza mfalme kuwa hapo getini kuna mtu mchafu anadai yeye ni mfalme, anahitaji kuingia ndani. Kumbe baada ya Mfalme kupotea, taarifa iliyotolewa na serikali ilielezwa kuwa mfalme amefariki, kwahiyo utawala ukachukuliwa na waziri mkuu wake. Mfalme mpya alipopata taarifa ya ujio mtu huyu alitoa amri apelekwe gerezani kwa kujaribu kufanya uhaini, akakamatwa na kwenda kutupwa Gerezani. "KIZUIZINI" ITAENDELEA..... Cc mzee wa liver, myambendi, khalidoum
 
Aiseee safi sana
 
Hahaha a has
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…