Conte, 48, aliwaambia wanahabari: "Nimeongea naye na nadhani Charly anatambua kosa lake. Kwa kweli nadhani anahitaji kuendelea kujitahidi sana kujiimarisha na hasa kifiziki. Akili yake inapaswa kuwa dimbani, siyo kwenye mitandao ya kijamii. Nimemwambia hili.
"Jukumu langu ni kumsaidia kupita njia sahihi, si njio ya upotevu. Zaidi ya yote unapokuwa na wachezaji wadogo ni muhimu kuzungumza naye, kuwaeleza namna ya kuchagua njia sahihi. Nimefanya hili na naamini ameelewa. Sioni tatizo lolote kwake.