Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b0ba2b50d04764a02c53ae870df7684f.jpg
 
Kusahau sana ni hali inayoweza kumfanya mtu akajichukia sana, kukosa raha na kua na mawazo sana afanye nini kupambana na adha hiyo..

Hii ni hali ambayo inaathiri watu wengi sana yaani wakubwa na wadodo kulingana na chanzo lakini inakua mbaya zaidi mtu anavyozidi kuongezeka umri kwani seli za ubongo zinazidi kupungua zaidi.
 
Kuna hali kitaalamu inaitwa dementia ambayo hutokea mara nyingi katika umri mkubwa na huambatana na kusahau kuliko pitiliza yaani kupotea katika mazingira unayoyafahamu, kusahau majina ya kawaida kabisa kama embe, pazia, kiti na meza, kurudia kuuliza swali la aina moja kila siku, na kuchanganyikiwa lakini hali huu huletwa na magonjwa Fulani mfano Alzheimer's disease{hii hali ni hatari na hutibiwa kitaalamu}
 
Lakini watu wengi hawafiki huko, ila watu wengi sasa wanasahau vitu vya kawaida sana yaani unakuta mtu kaenda na baiskeli au gari sehemu afu karudi kwa mguu na kuvisahau huko, mtu anasoma sasa hivi afu akifunika kitabu amesahau, unaweka pochi sehemu unasahau uliweka wapi, unameza dawa afu baadae hukumbuki kama ulimeza au vipi, unasahau pesa mfukoni, unapewa kazi afu unasahau kuifanya na kadhalika..
 
Kukosa usingizi: binadamu anatakiwa apumzike mpaka masaa nane kwa siku moja, lakini kutokana na ugumu wa maisha watu hujikuta wanalala mpaka masaa manne kwa siku. Hii huathiri uwezo wa kufikiri na kusahau kirahisi sana.
 
Madawa: dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali hua na madhara madogo madogo ambayo yanaleta kusahau.. mfano dawa za kutibu presha kama captopril, dawa za kutibu madonda ya tumbo mfano cimetidine na dawa za kutibu mgandamizo wa mawazo mfano amitriptyline.
 
Ulevi: unywaji wa pombe uliopitiliza huharibu uwezo wa kumbukumbu za mda mfupi yaani kusahau kitu umekifanya mda huo huo hivyo inashauriwa kunywa pombe kiafya. Yaani bia mbili kwa siku mwanaume na bia moja kwa siku mwanamke ambazo hazina alcohol zaidi ya asilimia tano zinatosha kiafya.
 
Back
Top Bottom