kutishia kujiua; zaidi ya 75% ya watu wanaotaka kujiua watatoa vitisho kwamba siku moja nitajiua, katika hali ya kawaida mtu unaweza ukapuuza ukidhani ni masihara lakini nakwambia ukioana mtu anatishia kujiua basi usipuuze kauli zake kitaalamu inaitwa 'call for help' kwamba anaomba msaada ili asijiue na hii ndio dalili kuu muhimu kuliko zote.
kuanza kujiaandaa; mtu anayetaka kujiua ataanza maandalizi kwa kugawa baadhi ya mali zake, kuwatembelea ndugu na jamaa, kuandika usia wa mali zake, kuandika barua ya chanzo cha yeye kujiua, na huweza kunua vitu vya kujiua kama dawa, sumu, bunduki au kamba.
je kujiua kunaweza kuzuilika?
ndio mtu anayetaka kujiua mara nyingi anakua anataka msaada, jaribu kukaa na kumuuliza kitu gani kinamsumbua na kama amefikiria kujiua..
mshauri kwamba matatizo hayapo kwa ajili yake tu kwani kuna watu wengi wenye matatizo zaidi yake na kikubwa ni kuvumilia kipindi hiki kigumu lakini pia msaidie kwenda hospitali au kituo chochote akaonane na mshauri, kama una nafasi ya kumsaidia basi msaidie kulingana na tatizo lake..
nifanye nini kumsaidia mtu anayetaka kujiua?
ukishagundua mtu anataka kujiua kuna mambo ya msingi sana unatakiwa kuyafanya ili kumsaidia asijiue kama ifuatavyo.
usimuache peke yake; hakikisha unakaa naye muda wote na ikiwezekana piga simu kwa ndugu na jamaa na marafiki ili wakusaidie.
nifanye nini kumsaidia mtu anayetaka kujiua?
ukishagundua mtu anataka kujiua kuna mambo ya msingi sana unatakiwa kuyafanya ili kumsaidia asijiue kama ifuatavyo.
usimuache peke yake; hakikisha unakaa naye muda wote na ikiwezekana piga simu kwa ndugu na jamaa na marafiki ili wakusaidie.
weka mbali vitu vya hatari; kama kuna kamba, au silaha yeyote basi ficha mbali lakini pia mwambie muhusika kwamba kama kuna kitu chochote ameshenunua kujidhuru basi mwambie akukabidhi uviweke mbali,
wasiliana na daktari ; kama ni mgonjwa wa akili ambaye anafahamika siku nyingi basi mpigie simu daktari wake ili aweze kurudishwa hospitali na kulazwa kabisa na kama hua sio mgonjwa wa akili basi apelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi.
mwisho; huenda wewe msomaji ndio muhusika ambaye umekata tamaa na unataka kujiua, nikupe moyo kwamba matatizo hayakuumbwa kwa ajili yako tu...kuna watu wengi wana matatizo makubwa zaidi yako na wengine waliwahi kua kwenye matatizo kama hayo na sasa wana mafanikio makubwa..usijiue hata kama umepata aibu au tatizo kubwa kiasi gani maishani mwako. kama ni mpenzi utapata mwingine, kama ni mtaji utapata mwingine, kama ni ugonjwa wewe sio wa kwanza kuugua hivyo jifunze kupambana nao...kumbuka muda ndio daktari mkuu yaani wazungu wanasema time will heal you
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.