Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Karoti hupatikana kwa wingi sokoni na magengeni japokuwa wengi wetu huwa tunaziona tu na hata wengine tunazinunua na kuishia kuzila kwenye michuzi ya nyama na vyakula vingine, Bei yake huwa ya kawaida sana kulingana na hali ya vipato vyetu lakini huwa na faida nyingi muhimu kwa afya zetu. Zinatupa manufaa mengi kuliko gharama kama inavyoelezwa hapo chini;
 
Huifanya ngozi iwe nzuri na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nazi au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka,
 
karoti hupunguza hatari ya kupata SHINIKIZO LA DAMU (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (blood vessels) na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…