Baada ya ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya Njombe Mji, kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka Dar es Salaam, kuelekea Visiwani Zanzibar, kwa ajili ya kuweka kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, dhidi ya Yanga.
Msemaji mkuu wa Simba, Haji Manara, ameiambia Goal, timu hiyo itaondoka Dar es Salaam saa 3 asubuhi na itawasili Zanzibar majira ya saa 5, na moja kwa moja wataingia kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi kwenye uwanja wa Aman Zanzibar.