Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kilimanjaro_mountain_mount_0025_summit_view_from_mountain_top_uhuru_peak_boeing_747.jpg
 
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo(stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi,kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.
 
Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.
 
Magonjwa ya moyo-Watu walio na msongo(Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo. Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.
 
Uzito mkubwa ambao hutokana na kusanyiko la mafuta katika eneo la tumbo (kitambi), ni hali hatarishi kiafya ukilinganisha na mkusanyiko wa mafuta katika miguu au makalio na ni bahati mbaya kuwa, watu wenye msongo huifadhi kiasi cha mafuta zaidi mwilini ukilinganisha na wale wasio na msongo . Hii ni kwa sababu, katika hali ya kuwa na msongo homoni ya cortisol hutolewa zaidi na hii husababisha mkusanyiko katika eneo hilo la tumbo.
 
Pumu-Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, msongo huzidisha maradufu, na hata kuwa kisababishi cha shambulizi la pumu. Katika utafiti mmoja uliofuatilia jinsi msongo kwa wazazi unavyochochea pumu kwa watoto, mfano kwa mama mjazito mwenye msongo aliyekuwa anavuta sigara. Matokeo ya tafiti hizo ni kuwa, watoto wenye wenye wazazi wenye msongo, walikuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa pumu ukilinganisha na watoto walioishi na wazazi wenye utulivu.
 
Ugonjwa wa kisukari waweza kusababishwa na msongo kwa namna mbili. Moja tabia mbaya ya kula kupita kiasi au unywaji wa pombe kupindukia wakati mtu ana msongo. Pili, msongo husababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari mwilini na kuchochea aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari.
 
Sononi na wasiwasi-Tafiti nyingi zimeonyesha uhusiano kati msongo sugu na kuwa na ugonjwa wa sononi pamoja na wasiwasi. Tafiti nyingi pia zimeonyesha kuwa, matatizo mengi ya sononi na wasiwasi yanatokana na masuala yahusianayo na kazi pamoja na matatizo ya kifamilia.
 
Back
Top Bottom