Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, ni kuwa ulaji wa angalau gramu 400(pungufu kidogo ya nusu kilo) za matunda na mboga kwa siku zinatuepusha na hatari ya kupata magonjwa yanayosumbua jamii nyingi duniani hivi leo. Magonjwa haya zaidi ni yale yasiyo ya
uambukizi kama kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na mengine mengi. Pia ulaji wa matunda na mboga mboga utatusaidia kupata viini lishe kama fiba, vitamini, madini katika viwango sahihi vinavyohitajika kwa siku.
 
Katika nchi zinazoendelea ambapo walio wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ni vigumu kuweza kumudu kufikia kiwango kilichopendekezwa na shirika la afya duniani, lakini hii isitufanye kushindwa kumudu kiwango kilichopendekezwa. Tunaweza kujitosheleza kwa matunda na mboga za majani kwa kuotesha miti ya matunda mbali mbali majumbani mwetu, pia kuwa na bustani za mboga mboga. Hii itatusaidia kuweza kufikia kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya WHO na kuboresha afya zetu.
 
Ili kuboresha kiwango kinachohitajika cha matunda na mboga mboga, basi hatuna budi kufanya

yafuatayo:-
Tuhakikishe kuwa nyumbani kwetu hapakosekani bustani za mboga na matunda.
Kila wakati hakikisha katika mlo wako haukosi mboga za majani.
 
Vitamini hii muhimu husaidia mmeng'enyo wa vyakula vya wanga, kuongeza uwezo wa ufanyaji kazi wa ubongo na kujifunza, husaidia kuepukana na msongo wa mawazo, husaidia hufanyaji kazi wa misuli ya moyo na mfumo wenye afya
wa mishipa ya fahamu.
 
Upungufu wa vitamini B1 hupelekea mtu kupata ugonjwa ujulikanao kama Beriberi. Mtu mwenye ugonjwa huu hupungukiwa na hamu ya kula, maumivu katika viungo vya ncha vya mwili (kitaalam kama peripheral neuropathy),kifua kubana, matatizo ya moyo na tatizo lijulikanalo kama Wernicke-Korsakoff Syndrome ambalo mtu hupata dalili zifuatazo:-
 
Zaidi ya watu milioni moja huambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku ulimwenguni kote. Inakadiriwa kila mwaka takribani watu milioni 500 huambukizwa moja ya magonjwa manne ya zinaa yaambukizwayo kwa kufanya ngono: Clamydia, kisonono, kaswende na trichomoniasis. Zaidi ya kinamama milioni 290 wameambukizwa maradhi yasababishwayo na HPV( Human Papilloma Virus), moja ya maradhi haya ya zinaa yaliyotamalaki sana na ambayo yanalaumiwa kwa kusababisha saratani ya shingo ya uzazi.(WHO).
 
Kipindupindu ni ugonjwa wa uambukizi ambao husababisha kuhara na kutapika ambao mtu hupata baada ya kunywa maji au kula chakula kilichochafuliwa na kinyesi au matapishi yenye aina ya bakteria wajulikanao kama Vibrio cholerae.
 
Katika karne ya 19, ugonjwa wa kipindupindu ulisambaa duniani kutoka huko ulikoanzia katika delta ya Ganges nchini India. Ugonjwa ulifika barani Afrika mwaka 1971 na huko Amerika mnamo mwaka 1991. Kipindupindu ni ugonjwa unaoathiri nchi nyingi duniani hivi leo.

Ugonjwa wa kipindupindu ni ambao humshambulia mhanga katika muda mfupi baada ya kuambukizwa, na huathiri watu wazima na watoto na huweza kusababisha kifo katika muda wa saa chache baada ya mgonjwa kuonyesha dalili za ugonjwa.
 
Katika karne ya 19, ugonjwa wa kipindupindu ulisambaa duniani kutoka huko ulikoanzia katika delta ya Ganges nchini India. Ugonjwa ulifika barani Afrika mwaka 1971 na huko Amerika mnamo mwaka 1991. Kipindupindu ni ugonjwa unaoathiri nchi nyingi duniani hivi leo.

Ugonjwa wa kipindupindu ni ambao humshambulia mhanga katika muda mfupi baada ya kuambukizwa, na huathiri watu wazima na watoto na huweza kusababisha kifo katika muda wa saa chache baada ya mgonjwa kuonyesha dalili za ugonjwa.
 
Utafiti unaonyesha asilimia 80% ya wanaoambukizwa huwa hawaonyeshi dalili ya ugonjwa, lakini bakteria wa ugonjwa huendelea kutolewa katika kinyesi kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi baada ya kuambukizwa na kuendelea kusababisha hatari ya kusambaa kwa ugonjwa. Wagonjwa wanaoonyesha dalili, huarisha maji yafananayo na maji ya mchele na huambatana na upotevu mkubwa wa maji mwilini ambao waweza kusababisha kifo mgonjwa asipotibiwa.

Kusambaa kwa ugonjwa wa kipindupindu kunahusishwa kwa karibu na utunzaji duni wa mazingira. Maeneo ambayo watu wake huwa katika hatari ya kupata ugonjwa ni yale yasiyopangwa na yenye msongamano mkubwa wa watu, pia katika kambi za wakimbizi ambapo ndipo penye miundo mbinu duni mfano mifumo ya maji safi, mifumo ya maji taka,ukosefu wa vyoo na hali ya usafi huwa ni ile iliyo duni kabisa.
 
Kipindupindu ni ugonjwa ulio tishio kwa afya ya jamii nyingi duniani na ni kiashiria muhimu kinachoonyesha jamii yenye maendeleo yaliyo duni.

Ili kujikinga na ugonjwa huu ni vyema kila mmoja wetu kuchukua hatua madhubuti.Serikali zinahitajika kuboresha maisha ya watu wake ikiwemo upatikanaji wa huduma bora za afya, maji safi,kuboresha miundo mbinu pamoja na kutoa elimu ya afya itakayosaidia watu kufahamu ugonjwa huu na jinsi ya kuepukana nao.
 
Back
Top Bottom