Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Hatua ya kwanza ukisha chukua nguo zako chafu namna hiyo ni kuziweka katika mafungu mafungu kabla ya kuanza kuosha. Nguo nyeupe zinakaa fungu lake, nguo zenye rangi nyeusi, dark blue, dark brown, dark grey etc(yani dark colours) na zenyewe fungu lake. Nguo ambazo ni chafu sana, au nguo delicate mfano gauni la lace material (lace dress), au nguo zinazotoa rangi , nguo za namna hiyo nazo kundi lake. Wakati unafanya zoezi hilo la ku sort nguo pia unapekua mifukoni kuangalia kama kuna kitu kimesahaulika kwenye mifuko ya nguo hizo, na kuangalia kama kuna nguo yenye doa.