Kwa mujibu wa The Mirror, Real Madrid wamebadili mawazo yao juu ya mchezaji huyo, 28, baada ya kusisitiza kuwa wanataka kuendelea kumbakisha klabuni mwao, na sasa wapo tayari kusikiliza ofa.
Habari zinadai kuwa Bale huenda akapokea ofa kutoka kwa klabu yake ya zamani Tottenham Hotspur na Man United ya Jose Mourinho, na inaaminika watabadilishana na Harry Kane.