Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jaribu kukaa chini angalia ni sehemu gani umeingiziwa hofu.woga, wasiwasi na ukashindwa kujitambua , umeshindwa kuona fursa. Ni wapi ulikoingiziwa hizo shida. Je ni nyumbani, kanisani, msikitini, shuleni au barabarani? Ukijua, Anza sasa hivi kuondoa hofu, wasiwasi, mashaka kwa kutafuta maarifa. Tafuta semina mbalimbali nenda kajifunze uondoe ujinga.
 
Uwe mtu wa Imani , Imani ni jicho la Mungu. Bila Imani huwezi kumpendeza Mungu. Hatuendi kwa woga bali kwa imani. Ukitaka kuwa na akili iliopevuka , jitahidi kutunza akili yako, nguvu zako, hisia zako, na fikra au mawazo yako.
 
badilisha mitazamo yako, kuwa mtu wa mitazamo mizuri, kinywa cha ukaidi ukitenge mbali na wewe na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe. Kuwa mlinzi wa mawazo yako ili mtu asije akakuingizia mambo mabaya yakakubomoa. Kuwa makini na yale unayoyasikia, unayoyaona na kuyahisi, kuwa makini na matendo yako.
 
Sasa kama ukiwa mtu mzima, ndio tunatambua kuwa tunahitaji utulivu zaidi kuliko tunavyofikiria , Kuna mambo mengi Ulimwenguni, Majukumu ya maisha, mara mambo ya mitandao , mikutano mingi wengine, kukosa muda wa kutuli peke yako. Hii bado ni kazi ya nidhamu , inabidi kujifunza iwe ni sehemu ya maisha yetu. Inabidi kuchagua utulivu mara nyingi.
 
Ni kwa vipi utulivu ni wa muhimu?



Kwa sababu ya mambo mengi yanatuweka kuwa bize, Ni muhimu kujitolea muda kwa ajili ya kukaa kwa utulivu ili kusikia kutoka kwa baba yetu. Anajali kuhusu mambo yanayoendelea kati yetu na hataki chochote kwetu zaidi ya kumkabidhi kila kitu na kumruhusu aongee kuhusu maisha yetu kwenye kila hali.
 
Anatutaka tuwe na mahusiano naye, hataki maneno mengi. Sio tu siku ya Jumapili au Ijumaa au Jumamosi Bali ni siku zote.

Ni wakati wa utulivu tu ndio neno la Mungu linaweza kuingia ndani ya mioyo yetu na kutupatia amani iliyo ya kweli na kutushangaza uelewa wetu. kwa kuwa amani hiyo inapita akili zetu na kuhifadhi mioyo na nia zetu.

Lakini tunawezaje kutuliza akili zetu kama kila kitu kinasukumwa na Nia zetu?
 
1.Vitendo



Itachukua muda kuzoea na kujifunza jinsi ya kutuliza akili zetu. itaonekana kama kitu kisichowezekana mwanzoni, Lakini Amini kwamba process yake ni kubwa na itakupa kitu kizuri cha kila siku.Kujitahidi kutulia itatusaidia kufahamu hata vitu ambavyo vinakula muda wetu bila sababu. Kama television, mitandao, Simu . Kipi ambacho unaweza kuachana nacho ili upate muda wa kutulia Na Mungu wako?
 
Kuna hitaji la kukutana na Mungu na kuwa na utulivu wa kusikia kutoka kwake. Hakuna mtu mwingine anahitajika muda huo… Ni muda wa kuongea na Mungu tu. Ni wakati wa kumshukuru kwa aliyofanya kwetu na pia ni muda wa mahojiano naye.
 
Back
Top Bottom